Klabu ya Rotary ya Jijini Dar Es Salaam leo imekabidhi rasmi wodi ya watoto wenye saratani kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili. Wodi hiyo imejengwa na Klabu hiyo kwa kiasi cha Shilingi Billioni 1.2 ikiwa ni gharama za ujenzi, samani, na vifaa tiba vya wodi hiyo. Wodi hiyo ni ya kwanza kwa ubora Kusini mwa Jangwa la Sahara. Tafadhali fuatilia katika picha yaliyojiri wakato wa ufunguzi
Hii ndiyo wodi iliyojengwa na Klabu ya Rotary kwa kushirikiana na wadau wengine. Ni sakafu moja ya juu ambayo imewekwa bango.
Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, akifuatiwa na Mgeni rasmi Dr. Jane Goodall aliyeko kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Sr. Agnes Mtawa wote kwa pamoja wakipokea ufunguo wa wodi hiyo kutoka kwa watoto wanaougua saratani.
wageni mbalimbali wakifuatilia kwa karibu hotuba mbalimbali wakati wa ufunguzi.
Wageni wakitembelea wodi kuona ilivyojengwa.
No comments:
Post a Comment