Wednesday, 21 August 2013

RECIPE YA JUISI YA KABICHI HUTIBU VIDONDA VYA TUMBO NA SARATANI.

 

kabichi_36d0e.jpg
VIDONDA vya tumbo ni ugonjwa ambao umekuwa ukiwasumbua watu kadhaa na hata kusababisha kifo kutokana na vidonda kuwa vikubwa, utumbo kuharibika, kupoteza damu nyingi na kupatwa na saratani.
P.T

Mojawapo ya njia za asili za kupambana na ugonjwa wa vidonda vya tumbo pamoja na aina fulani za saratani kama vile sarafani ya korodani, matiti na utumbo mk
ubwa, ni kwa kutumia juisi inayotengenezwa kutokana na kabichi. 

Walioitafiti wanasema kabichi ina uwezo wa kupambana na asidi ya tumboni kwa kuwa ina L-glutamine na gefarnate ambazo zinalinda ngozi laini ya viungo vilivyotajwa hapo juu.

Juisi ya kabichi pia inawafaa wanaopenda ngozi zao ziwe nyororo ikiwa wataichanganya kwa karoti ama asali na hata hamira, kisha wakajipaka kwenye ngozi na kusubiri dakika 15 kabla ya kusafisha kwa maji.

Mahitaji:
Kabichi ya ukubwa wa wastaniMaji safi na salama yaliyochemshwa na kuchujwa ili kupunguza chumvi chumvi (au tumia distilled water).


Kisu cha kukatiaMahali pa kukatiaBlender ya kuchanganyaChupa yenye mfuniko kwa ajili ya kuhifadhiaChujio/chekeche
Njia:
2_4a155.jpg3_06327.jpg
Kata kabichi na kujaza vikombe vitatuOngeza maji vikombe viwili kwenye kabichi iliyokatwaChemsha mchanganyiko huo katika moto wa wastani kwa dakika 25 hadi nusu saa hivi.

Weka mchanganyiko wako huo kwenye blender (kama ni kubwa weka mara moja, kama ni ndogo weka kidogo kidogo) kisha washa blender ifanye kazi yake kulainisha kidogo tu kabichi ila isiwe rojo rojo.

Mimina mchanganyiko wako kwenye chupa ya kuhifadhia na kisha ifunike ili hewa isiingie ndani (ikibidi weka nailoni kwenye mdomo wa chupa kabla ya kukaza kifuniko)Ihifadhi chupa hiyo kwenye sehemu ya kawaida (room temperature, siyo kwenye jokofu/friji) na iache itulie hivyo kwa siku kati ya 3 hadi 5 ili ichachuke (fermentation). 

Hatua hii inasaidia bakteria wenye manufaa (kama wanaochachusha maziwa mgando/mtindi) kufanya kazi inayotakiwa vyema ili juisi iwe na nguvu inayohitajika katika mfumo wa mmengenyo wa chakula, tumboni, utumbo n.k.

Siku ya tatu au ya nne ama ya tano, chukua kichujio (chekeche), faneli (funnel) na chupa nyingine kisha chukua ile yenye mchanganyiko uliouhifadhi, ifungue (itakuwa inatoa harufu inayonuka kwa sababu ya kuchachuka), kisha anza kuchuja kwa kumimina juisi iliyomo kwenda kwenye chupa isiyo na kitu.

Juisi yako ni tayari kunywewa na unaweza sasa kuihifadhi kwenye jokofu/friji ipate ubaridi unaoutaka na vile vile kuzuia isiendelee kuchachuka haraka zaidi kama awali.

Makapi ya kabichi uliyochuja unaweza kuyahifadhi kwa matumizi tena ya siku inayofuata kwa kuyaongezea kikombe kimoja cha mchanganyiko mpya na kuacha yakae tena kwenye joto la kawaida (room temperature) kwa siku moja (kwa kuwa tayari kiasi kikubwa kimeshachachuka) na kuyachuja siku inayofuatia ili kupata juisi nyingine.
Source: http://www.wavuti.com

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!