Mkurugenzi Kitengo cha Mawasiliano, SIKIKA, Bi. Lilian Kallaghe, akiteta jambo na wachoraji nje ya Jengo la Watoto, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, Jumamosi iliyopita, walipokutanishwa na mradi wa kujitolea wa Wafanye Watabasamu, uliobuniwa na Nathan Mpangala. Mradi huo ulikwenda kuwafariji, kuwapa zawadi kisha kuchora na watoto wanaoendelea na matibabu ya saratani hospitalini hapo, ikiwa ni sehemu ya tiba ya saikolojia. Kutoka kushoto Gadi Ramadhan (Art director), Nathan Mpangala (ITV, Mratibu Wafanye Watabasamu), Said Michael ‘Wakudata’ (Tanzania Daima) na Abdul King O ‘Kaboka Mchizi’ (Nipashe). Mengi kuhusiana na mradi huu, bofya; https://www.facebook.com/pages/Wafanye-Watabasamu-Make-Them-Smile/140812046112398. Picha zote: Wafanye Watabasamu.
Mratibu wa mradi wa kujitolea wa Wafanye Watabasamu, Katunisti Nathan Mpangala ‘Kijasti’ (mwenye kijibegi mgongoni), akisaidiana na familia, ndugu, jamaa na marafiki kuteremsha zawadi kwa ajili ya watoto wanaoumwa saratani, Jumamosi iliyopita, Hospitali ya Taifa Muhimbili. Karibu na ‘Kijasti’ kulia ni ‘Mama Kijasti’. Baadhi ya watoto wanaotibiwa saratani, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam, wakionesha uhodari wa kuchora wakati walipotembelewa na mradi wa Wafanye Watabasamu, unaoratibiwa na Nathan Mpangala, Jumamosi iliyopita. Watoto hao wapatao 80, walizawadiwa sabuni za kuogea/kufulia, dawa za meno, biskuti, toilet papers, mafuta ya kupakaa, matunda na vifaa mbalimbali vya kuchorea toka kwa marafiki wa mradi huo. Zaidi bofya; https://www.facebook.com/pages/Wafanye-Watabasamu-Make-Them-Smile/140812046112398 Wachora vibonzo, Nathan Mpangala ‘Mtukwao’ wa ITV, (kulia) na Abdul King O ‘Kaboka Mchizi’ wa Nipashe, wakichora na malaika wanaoendelea na matibabu ya saratani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam, Jumamosi iliyopita, wakati wa ziara ya mradi wa Wafanye Watabasamu, hospitalini hapo. Mengi kuhusu zoezi hili, tembelea; https://www.facebook.com/pages/Wafanye-Watabasamu-Make-Them-Smile/140812046112398 Rafiki wa Wafanye Watabasamu ambaye pia ni katunisti wa magazeti ya Mwananchi, Masoud Junior, akishuhudia umahiri wa kuchora toka kwa baadhi ya watoto wanaoendelea na matibabu ya saratani katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam, juzi, wakati wa ziara ya mradi wa Wafanye Watabasamu. Ilikuwa jambo la kutia moyo kuona watoto hawa wanasahau maumivu ya saratani kwa muda na kujikita kwenye uchoraji. Mratibu wa Wafanye Watabasamu, Nathan Mpangala, anawashukuru wachoraji wenzake, ndugu na marafiki wote waliochangia muda, sadaka na tabasamu kwa watoto hao. Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Shirika lisilo la Kiserikali la SIKIKA, Bi. Lilian Kallaghe, (kushoto), yeye aliamua kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa kuungana na marafiki wa Wafanye Watabasamu, ili kuwafariji watoto waoendelea na matibabu ya saratani katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam, juzi.
No comments:
Post a Comment