Saturday, 17 August 2013

MWISHO WA HABARI HII YA HERUFI ZA MAJINA YETU NA MAANA ZAKE, KUTOKA KWA WAJUZI WA MAMBO! SOMA HERUFI YANGU HAPO! AM BLESSED AISEE!

Horoskopbild

 

 

HERUFI O  Mwenye jina linaloanzia na herufi O ni mtu mwenye subra, mvumilivu na mwenye bidii ya kusoma. Ni mtu mwenye kupenda kutumikia jamii na mwenye uwezo mkubwa wa kudhibiti hisia. Herufi O inawakilisha Nyota ya Mapacha

 

HERUFI P Mwenye jina linaloanzia na herufi P ni mtu mwenye uwezo wa kuamrisha na hekima kubwa. Ana nguvu za kiroho lakini anapenda sana kujitumbukiza kwenye mambo ya watu. Herufi P inawakilisha Nyota ya Kaa

 

 HERUFI Q Mwenye jina linaloanzia na herufi Q ni mtu mwenye kupenda mambo ya asili. Ni watu wasiyoelezeka nawana uwezo wa kuonyesha vitu visivyojulikana hata hivyo ni mtu aliyepooza sana. Herufi Q inawakilisha Nyota ya Simba

 

 

 HERUFI  Mwenye jina linaloanzia na herufi R ni mtu mwenye uvumilivu, wenye huruma lakini ana hasira za haraka. Muda wote anakuwa mpenda amani. Herufi R inawakilisha

 

 Nyota ya Mashuke

 
 

 HERUFI S Mwenye jina linaloanzia na herufi S ni mtu mwenye mvuto mkali wa kuleta utajiri. Ni watu wenye maamuzi ya ghafla na hupenda mageuzi makubwa. Herufi S inawakilisha Nyota ya Mizani

 
 

 HERUFI T Mwenye jina linaloanzia na herufi T ni mtu mwenye kupenda ushauri wa kiroho, anatumia nguvu za ziada kusaidia watu na hupata mafanikio baada ya muda mrefu. Ni watu wenye hisia kali sana na ni wepesi kushawishika. Herufi T inawakilisha Nyota ya Nge

 

 HERUFI U Mwenye jina linaloanzia na herufi U ni mtu mwenye bahati kubwa kwa ujumla. Anapenda uhuru katika mapenzi. Lakini ni mtu mbinafsi, mwenye tamaa na aliyekosa maamuzi. Herufi U inawakilisha Nyota ya Mshale.

 
 

 HERUFI V Mwenye jina linaloanzia na herufi V ni mtu Mchapakazi, wenye bidii na asie choka. Hata hivyo ni watu wasiotabirika. Herufi U inawakilisha Nyota ya Mbuzi.

 
 

 HERUFI W Mwenye jina linaloanzia na herufi W ni mtu muwazi, wachangamfuu kupita kiasi na mwenye uwezo wa kutambua mtu mwema na mbaya. Ni watu wenye tamaa na hufanya mambo ya hatari. Herufi W inawakilisha Nyota ya Ndoo.

 
 
 

 HERUFI X Mwenye jina linaloanzia na herufi X ni mtu asiyependa kuwekewa vizuizi katika kwenye anasa na ni rahisi kujiingiza kwenye uzinzi na kujitoa uaminifu. Herufi X inawakilisha Nyota ya Samaki.

 

 HERUFI Y (YASINTA) Mwenye jina linaloanzia na herufi Y ni mtu mwenye kupenda Uhuru na hawapendi kupingwa jambo lao lolote. Ni watu wanaokosa uamuzi na husababishia kupoteza bahati katika maisha. Herufi Y inawakilisha Nyota ya Punda

 
 

HERUFI Z Mwenye jina linaloanzia na herufi Z ni mtu mwenye kupenda matumaini na amani. Ni wenye msimamo mkali ila wanashauriwa kufikiria kabla ya kuamua jambo. Herufi Z inawakilisha Nyota ya Ngombe.


No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!