Alexander Kinyua (kushoto) na mwanamume aliyekuwa akiishi naye nyumba moja Kujoe Bonsafo Agyei-Kodie.
MWANAFUNZI
kutoka Kenya aliyekuwa akiishi Marekani amekili kwamba alimuua
mwanamume waliyekuwa wakiishi nyumba moja na kula moyo wake na ubongo
wake.
Alexander
Kinyua, 22, alikiri mashtaka ya mauaji ya Kujoe Bonsafo Agyei-Kodie,
37, katika jimbo la Maryland mwaka jana lakini Jaji akasema hafai
kulaumiwa aliposhtakiwa Jumatatu wiki hii.
Jaji
Stephen Waldron alisema Kinyua hawezi kulaumiwa kwani alikuwa anaugua
akili na akaagiza awekwe kwenye hospitali ya watu wenye akili punguani.
Kinyua,
aliyekuwa mwanafunzi wa uhadhisi katika chuo cha Morgan State, aliambia
maafisa kwamba alitumia kisu kuua mwenzake kabla ya kula viungo vyake.
Agyei-Kodie, mzaliwa wa Ghana, aliishi na Kinyua nyumba moja kwa wiki sita kabla ya kutoweka kwake Mei 2012.
Kinyua
awali alikana kujua kuhusu kifuo cha mwenzake, lakini mwishowe
akawapeleka maafisa hadi jaa la kanisa ambapo alikuwa ameficha mwili wa
marehemu.
Dawa
Mauaji
hayo yalitokea Kinyua akiwa nje kwa dhamana kwa kumshambulia kwa mkwaju
wa kucheza besiboli mwanafunzi mwenzake wa zamani.
Kinyua alimwacha Joshua Ceasar mnamo Mei 19, 2012 akiwa karibu kipofu baada ya kumshambulia.
Mahakamani Jumatatu Kinyua alijibu maswali ya jaji kwa upole na alisema dawa ambazo amekuwa akipewa zimekuwa zikimsaidia.
Uchunguzi
wa hali yake ya kiakili ulibaini kuwa alikuwa anaugua ugonjwa ambao wa
Kiingereza hujulikana kama ‘paranoid schizophrenia
No comments:
Post a Comment