Stori: Makongoro Oging’ na Haruni Sanchawa
MTANDAO hatari wa unga nchini Tanzania umeshanaswa, kwa sasa unafanyiwa kazi kwa kasi na Kitengo cha Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya, chini ya kamanda wake, Godfrey Nzowa.
Habari njema kuhusu kunaswa kwa mtandao wa unga, zinakuja baada ya Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe kufanya kazi nzuri na kuwataja watu ambao inadaiwa walihusika katika kupitisha madawa ya kulevya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam.
Sekeseke kuu ni kukamatwa kwa Watanzania wawili, Agnes Gerald ‘Masogange’ ambaye ni mwanamitindo na Melisa Edward, nchini Afrika Kusini, wakiwa na madawa ya kulevya aina ya Crystal Methamphetamine, yenye uzito wa kg 120, Julai 5, mwaka huu.
Katika mtandao huo siri kubwa iliyovuja ni majina na jinsi biashara hiyo inavyoendeshwa Mkoa kwa Mkoa Wilayani mpaka Mitaani, vilevile wanamichezo na wasanii mbalimbali ambao imeshabainika kwamba wengi wao wanatumika kwa kusafirisha unga.
Imebainika kwamba mtandao huo umebainika baada ya watu 2,075 kukamatwa katika kipindi cha Januari hadi juni mwaka huu, ambao baadhi ya picha zao ndio hizo kama zinavyoonekana.
"Watu waliokamatwa kimsingi ni wale waliotumwa tu, sasa wale ndio wamewatajamabosi wao, wameeleza siri kubwa" alisema kamanda Nzowa.
GPL

No comments:
Post a Comment