Tuesday, 6 August 2013

MITINDO YA KIAFRIKA YATINGISHA LONDON.




Kulingana na waandalizi wa maonyesho hayo, lengo lao lilikuwa kusherehekea aina ya mitindo kutoka sehemu mbali mbali duniani na kuiweka fasheni ya Afrika katika ukumbi wa kimataifa . Mwanamitindo huyu anaonyesha vazi la muundaji LollyAde.
''Kuna waafrika wengi wenye talanta barani na pia katika nchi za kigeni, lakini changamoto wanayokabiliwa nayo ni ukosefu wa pesa na pia huwa hawana uwezo wa kuigeuza talanta yao kuwa biashara,'' asema Sinem Bilen-Onabanjo, kutoka miongoni mwa waandalalizi wa maonyesho hayo.
Maonyesho haya hutoa fursa kwa wanaounda mitindo hii kuonyesha dunia mitindo yao ambayo inaweza kuwaletea faida za kifedha

 
Muundaji aliyejifunza mwenyewe kutengeza mitindo Tumisola Ladega mwenye umri wa miaka 14 pekee (kulia) aliwashangaza wengi na mitindo yake.
"nilianza kubuni hii mitindo yangu miaka mingi iliyopita. Lakini haikuwa yenye hadhi ya juu.Lakini sasa imeweza kuwa yenye hadhi ya juu kwani tangu hapo nilianza kubuni zaidi na mitindo yangu ndio hii kama unavyoiona,'' alisema Ladega .
Haya ni maonyesho ya tatu ya mitindo ya kiafrika ...imekuwa ikifanyika katika mtaa wa Old Truman Brewery mjini London.
Jennifer Onah (kulia), ni mmliki wa kampuni ya kitindo ya Ferona, mjini London na anaitikia mizizi yake ya kiafrika, lakini mitindo yake pia ina sura za mitindo ya ulaya.
Mashabiki wengi waliofika walitumia simu na tabiti kunasa picha walizopendezwa nazo zaidi.
Wanamitindo wengi wanatumai kuwa kazi zao zitaweza kuonekana na waafrika ambao watapa soko kwa biashara zao
Agata Reis (kushoto), raia wa Angola, aliyehamia London akiwa mtoto mdogo, anasema anapata msukumo kutoka kwa vijana wa London anapounda mitindo yake ikiwemo, muziki wa afro-house na maswala ya kisiasa kama mapinduzi katika nchi za kiarabu.
Mbali na maonyesho, kulikuwa na pia waliokuwa wanaonesha mishono ya kiafrika na mapambo mengine

Wanamitindo chipukizi na waliokolea kutoka barani Afrika na kutoka nchi zengine za kigeni wamekuwa wakionyesha mitindo yao wakati wa wiki ya maonyesho ya mitindo ya kiafrika mjini London mwaka 2013. Ni picha zake mpiga picha wa BBC Manuel Toledo.

CHANZO: BBC SWAHILI

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!