Wednesday, 28 August 2013

KUTOKA JESHI LA POLISI TANZANIA:SOMA TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI KIDATO CHA NNE NA SITA 2013.



Jeshi la Polisi Tanzania limetoa majina na ratiba ya usahili kwa vijana waliomaliza kidato cha nne mwaka 2012 na waliomaliza kidato cha sita mwaka 2013 ambao wamechaguliwa kufanya usaili kabla ya  kujiunga na Jeshi la Polisi.

Mikoa, vituo na tarehe za usaili zimeoneshwa kwenye jedwali hapa chini:
NA
MIKOA
KITUO CHA USAILI
TAREHE ZA USAILI
MUDA WA  USAILI
1
KILIMANJARO  NA TANGA OFISI YA RPC TANGA02-04 /09/201308:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
2
MANYARA NA ARUSHAOFISI YA RPC ARUSHA06-09 /09/201308:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
3
RUVUMA  NA NJOMBEOFISI YA RPC NJOMBE12-14 /09/201308:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
4
IRINGA NA MBEYAOFISI YA RPC MBEYA16-18 /09/201308:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
5
RUKWA NA KATAVIOFISI YA RPC RUKWA20-23 /09/201308:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
6
MTWARA NA LINDIOFISI YA RPC MTWARA26-28 /09/201308:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
7
KIGOMAOFISI YA RPC KIGOMA02-04 /09/201308:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
8
MWANZA NA MARA OFISI YA RPC MARA06-09 /09/201308:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
9
GEITA NA KAGERAOFISI YA RPC  GEITA12-14 /09/201308:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
10
SHINYANGA NA SIMIYUOFISI YA RPC SHINYANGA17-19 /09/201308:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
11
TABORA NA SINGIDAOFISI YA OCD NZEGA21-24 /09/201308:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
12
MOROGORO NA DODOMAOFISI YA RPC DODOMA 26-28 /09/201308:00 ASUBUHI -16:00 JIONI
13
DSM NA PWANIDSM  POLICE  ACADEMY01-03 /10/201308:00 ASUBUHI -16:00 JIONI

Muhimu:
  • Mwombaji anaruhusiwa kufanya usaili kwenye kituo chochote cha usaili kilicho karibu naye kulingana na tarehe zinavyoonesha kwenye jedwali hapo  juu ili mradi tu awe amejiridhisha kuwa ni miongoni mwa walioitwa kwenye usaili. Jeshi la Polisi halitahusika na lawama yoyote ile kwa mtu atakayekwenda kwenye kituo cha usaili hali ambapo jina lake si miongoni mwa walioitwa kufanya usaili.
  • Mwombaji aliyeitwa kwenye usaili aje na vyeti vyake vyote vya masomo [(Academic Certificate(s)/Results slip(s) & Leaving certificate(s)], nakala halisi ya cheti cha kuzaliwa (Original Birth certificate). Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika.
  • Mwombaji  awe na namba ya simu itakayotumika kumjulisha endapo atachaguliwa..
  • Kila mwombaji aliyeitwa kwenye usaili atajigharamia usafiri, chakula na malazi kwa muda wote wa zoezi la usaili. Pia waombaji waje na kalamu za wino kwa ajili ya usaili wa kuandika.
Ni muhimu sana kwa kila mwombaji kuzingatia muda wa kuanza usaili.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!