Monday, 19 August 2013

HIVYO NDIVYO ILIVYOKUWA WAKATI SHEIKH PONDA ALIPOKWENDA MAHAKAMANI MJINI MOROGORO, AWASILI NA NDEGE YA POLISI, ULINZI MKALI WAIMARISHWA....

 
 
 
  
 
Sheikh Issa Ponda  Akiwasili Mahakamani Mkoani Morogoro Leo Asubuhii
 Mara baada ya kusomewa hukumu hapa akiondoka mahkamani na kurudishwa rumande mpaka tarehe 28
Akiwa kizimbani tayari kusomewa mashtaka yake yanayomkabili

Sheikh Issa Ponda Akiwa mahakamani mkoani Morogoro asubuhi ya leo  Sheikh Ponda Amesomewa Mashtaka Matatu katika Mahakama ya mkoa wa Morogoro Likiwemo la uchochezi alilolitoa Kwenye  Mkutano wa Hadhara Tarehe 10 mwezi huu Ambapo Inadaiwa alisema kwamba ''Ndugu waislamu Msikubali uundwaji wa kamati za ulinzi na usalama za Misikiti kwani kamati hizo zimeundwa na Bakwata ambao ni vibaraka wa Serikali ''katika viwanja vya shule ya kiwanja cha ndege Mkoani Morogoro.Baada ya kusomewa Mashitaka hayo Mahakama imesema Upelelezi Umekamilikaa Dhamana Imefungwa  na Amerudishwa Rumande Mpaka tarehe 28 mwezi huu ambapo kesi hiyo itaanza kusikilizwa katika Mahakama ya Mkoa wa Morogoro.





 


 

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!