Watu wawili wamefariki dunia na kumi wamejeruhiwa baada ya gari aina ya pickup mali ya kampuni ya hood iliyokuwa imebeba ndugu wa familia moja wakielekea msibani kuacha njia na kupinduka mara tatu katika eneo la kata ya mkuyuni wilayani morogoro .
Vilio na majonzi vilitawala katika hospitali ya mkoa wa morogoro mara baada maiti na majeruhi kuwasili
Ambapo ndugu wa marehemu wamesema waliofariki ni leila ngurungu pamoja na kaka yake aliyekuwa mchezaji wa siku nyingi katika soka idrisa ngurugu ambapo wamesema walikua njiani kwenda kwenye msiba wa kaka yao mkubwa ambapo njiani walipata ajali na kuwa chanzo cha ajali ni mwendo kasi huku baadhi wa ndugu wakieleza kuwa msiba huo ni pigo kwani wamepoteza ndugu watatu wa familia moja.
Nao majeruhi waliolazwa katika hospitali ya mkoa wa morogoro wakiziungumzia tukio hilo wamesema chanzo cha ajali ni dereva wa gari aina ya pickup aliekua akijaribu kukwepa ajali ya uso kwa uso na kisha gari kuacha njia na kupinduka mara nne.
Jeshi la polisi Mkoa wa morogoro limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na maiti zimehifadhiwa katika chumba cha maiti hospitali ya mkoa wa morogoro na majeruhi wanaendelea na matibabu
No comments:
Post a Comment