juu katika picha ni keki iliyotumwa na wafungwa katika ‘bethidei’ ya Mwigizaji Kajala Masanja,na chini
Kajala akishika sahani ya keki kwa ajili ya kumlisha Wema.
KATIKA hali ya kushangaza, baadhi ya wafungwa walio nyuma ya nondo za
Gereza la Segerea a.k.a Segedansi, Dar, wametuma keki ya ‘bethidei’ kwa
Mwigizaji Kajala Masanja ikiwa ni miezi michache tangu alipoachiwa huru
baada ya Wema Isaac Sepetu kumlipia faini ya Sh. milioni 13.
Tukio hilo lilijiri Jumatatu iliyopita Julai 22, mwaka huu ambapo
mwanadashosti huyo alikuwa akisherehekea siku yake ya kuzaliwa bila
kutaja umri aliofikisha.
Kabla ya pati hiyo na zoezi la kukata keki
ikiwemo iliyotumwa na wafungwa hao, iliyopangwa kufanyika wakati wa
kufuturu, Kajala aliianza siku hiyo kwa kwenda kutoa misaada kwa watoto
yatima.
Huku akiongozana na rafiki zake, Kajala alikata keki yake ya kwanza
katika Kituo cha Watoto Yatima cha Mitindo House Talent (MHT),
kilichopo Msasani, Dar, kinachomilikiwa na mbunifu maarufu wa mavazi,
Khadija Mwanamboka.
Baada ya kukata keki mbili ambazo alikwenda nazo
kituoni hapo, Kajala pamoja na wapambe aliongozana nao walikwenda moja
kwa moja nyumbani kwa Beautiful Onyinye au Madam Wema, Kijitonyama
jijini Dar ambapo shughuli nzima ilichukua nafasi wakati wa futari.Katika futari hiyo ambayo ilikuwa ni kwa ajili ya kusherehekea siku ya kuzaliwa ya Kajala, walialikwa watu mbalimbali huku kukiwa na vyakula vya kila aina wakiwemo mbuzi wawili wa kuchoma.
Baada ya futari watu walihamia kwenye ukataji wa keki zilizokuwa mezani zipatazo kumi na tano kutoka kwa marafiki wa Kajala huku Wema akiwa amenunua keki tano kwa ajili ya ‘shostito’, wake huyo.
Katika keki zote, iliyowafurahisha watu wengi ni ile iliyotumwa na wafungwa wa Gereza la Segerea iliyokuwa imeandikwa ‘Happy Birthday Mkuu wa Nyapara From Segerea Crew 2013’ ambayo kila mtu aliyeisoma alikuwa akicheka na kuanza kumtania mwanadada huyo kuwa ni Nyapara.
Kajala alisema kuwa Keki hiyo kutoka ilimkumbusha maisha ya gerezani lakini pia alifurahi kuona watu aliokuwa nao lupango humo kumkumbuka hivyo alifarijika kupita maelezo.
Kajala alitupwa gerezani wakati kesi yake na mumewe Faraji Agustino ya kutakatisha fedha haramu ikiunguruma ambapo baada ya hukumu, mwanadada huyo alitakiwa kwenda jela miaka mitano lakini alilipiwa faini na kurejea uraiani huku mumewe akienda