Monday 1 July 2013

WANATAFUTWA NA POLISI KWA YEYOTE ATAKAYEWAONA WATU HAWA ANAOMBWA ATOE TAARIFA KITUO CHOCHOTE CHA POLISI KILCHOPO KARIBU.






Jeshi la Polisi linazo taarifa za kuaminika kuhusu watu hawa, wanaoonekana katika hizo picha hapo juu, ambao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vikubwa vya kihalifu hapa nchini na katika maeneo mbalimbali nje ya nchi yetu.

 


Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi wote wazalendo na wenye mapenzi mema na nchi yetu, kutoa taarifa za watu hawa popote watakapoonekana katika kituo chochote cha Polisi kilicho caribú, ili waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye mkondo wa sheria.

 


Ndugu mwananchi, hata kama ni ndugu yako, usisite kutoa taarifa za watu hawa kwa sababu ni watu hatari sana. Zawadi nono itatolewa kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa watu hao.

Kwa taarifa unaweza pia kupiga Makao Makuu ya Polisi kwa kutumia simu namba 0754 78 55 57.

 


Imetolewa na

Advera Senso - SSP

 

Msemaji wa Jeshi la Polisi(T)






 
SOURCE. MICHUZI.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!