Saturday, 27 July 2013

"NILIJUA TU KWAMBA WANAFIKI WATAFURAHIA MATESO YANGU" ....AGNESS MASONGANGE


 



VIDEO Queen ambaye hivi karibuni alidaiwa kukamatwa na madawa yanayosadikiwa ni ya kulevya ‘unga’ nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’, Agness Gerald ‘Masogange’ amefunguka kuwa alijua watu wengi watafurahia kilichompata kwa kumuongelea kila wakati.

Akizungumza na mwanahabari wetu kwa njia ya simu akiwa Sauzi, Masongange ‘alishauti’ kuwa watu wengi wanamuongelea vibaya bila kujua nini kilichompata  hivyo anaamini hata marafiki zake wa karibu wamefurahia tatizo alilopata.


“Najua kabisa kuna watu wengi wamefurahia tatizo nililopata lakini watambue kuwa kila mtu anaweza kupata tatizo hivyo wapunguze kuongea sana bila kujua ni kitu gani kilichotokea juu yangu,” alisema Masogange ambaye atapanda kizimbani kwa mara ya pili mwezi ujao.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!