Wednesday 3 July 2013

NGASSA AANZA KUJIFUA RASMI NA TIMU YA YANGA


Na Khatimu Naheka

HATIMAYE kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa (pichani), amekata mzizi wa fitna baada ya kuanza kujifua rasmi na timu hiyo, ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu asajiliwe.

Awali kulikuwa na utata wa mchezaji huyo ataichezea timu gani kati ya Simba na Yanga ambazo zote zilikuwa zinadai kuwa zina mkataba na kiungo huyo, ilifika mbali mpaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lilisema kuwa bado linautambua mkataba wa Simba na mchezaji huyo mzaliwa wa Mwanza.

Lakini jana alionekana ni mchezaji wa Yanga baada ya kumaliza mkataba wa mkopo akitokea kwenye kikosi cha Azam aliokuwa akichezea, kwenye kikosi cha Simba.

GPL.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!