Thursday 4 July 2013

MFANYABIASHARA AGONGA WATU SITA NA GARI NA KUWAJERUHI VIBAYA.





Watu sita wamejeruhiwa vibaya ikiwemo kuvunjika baadhi ya sehemu mbalimbali za mwili huku mmoja wao akiwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali ya taifa ya Muhimbili baada mfanyabiashara (44) Mkazi wa Bahari Beach, kuwagonga kwa gari huko Bahari Beach. Chanzo kinaeleza kuwa mfanyabiashara huyo alifanya tendo hilo, baada ya kuwa na mabishano na rafiki yake wa kike,(MPENZI WAKE) ambaye walikuwa wakipata kinywaji pamoja, na ndipo mara baada ya mabishano hayo, mpenzi huyo wa kike aliondoka katika sehemu hiyo,tendo lililompelekea mfanyabiashara huyo kuchukua gari na kuwagonga watu wengine waliokuwa wamesimama pembeni.

 Kwa mujibu wa Kamanda Kova mfanyabiashara huyo amekamatwa kujibu mashitaka ya jinai

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!