Rais Kikwete akimkaribisha Rais wa Marekani Barrack Obama mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Julius Kambarage Nyerere leo mchana.
Rais Obama akikagua gwaride
Rais Obama akisalimiana na Rais wa Zanzibar Dr Alli Mohamed Shein
Makamu wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Idd akisalimiana na rais Obama
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi naUsalama nchini Tanzania, General Davis Mwamunyange, akisalimiana na Rais Obama, katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere
Rais Obama akifurahia midundo mbalimbali iliyokuwa ikitumbuiza.
Rais Barack Obama wa Marekani akisakata ngoma na rais Kikwete.
Rais Barack Obama wa Marekani amewasili Tanzania kwenye kituo chake cha mwisho katika ziara yake ya nchi tatu za Afrika. Bw. Obama alilakiwa na rais wa Tanzania Jakaya Kikwete na maelfu ya watu pamoja na kundi la wacheza ngoma na sarakasi katika uwanja wa ndege wa Dar es salaam Jumatatu.
Katika ziara yake ya siku mbili nchini Tanzania Bw.Obama atafanya mazungumzo na rais Kikwete, kukutana na viongozi wa biashara na kuzungumza na mkutano wa wakuu wa biashara nchini humo .
Tanzania ni moja ya nchi 9 ambazo zitazoshirikishwa katika juhudi mpya aliyotangaza rais Obama Jumapili kusaidia kuongeza nguvu za umeme barani Arika kusini mwa jangwa la Sahara.
Alitangaza mpango wa dola bilioni 7 katika hotuba yake katika chuo kikuu cha Cape Town huko Afrika Kusini na kusema itaongeza uzalishaji wa umeme maradufu kwenye bara hilo.
Pamoja na Tanzania juhudi hiyo itaanzishwa Ethiopia , Kenya , Liberia na Nigeria Uganda na Zimbabwe .
Jumapili rais Obama alitembelea kisiwa cha Robben ambako rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela alifungwa kwa miaka 18 kati ya miaka 27 aliyokuwa kifungoni kwa mapambano yake dhidi ya kupinga ubaguzi Afrika kusini.
No comments:
Post a Comment