ALI Omar, mkazi wa Kijiji cha Mabana, wilayani Kilosa, Mkoa wa Morogoro anashikiliwa na polisi kwa kosa la kumkata miguu Said Iddi kwa kumtuhumu kumfumania na mkewe aliyejulikana kwa jina la mama Ali, mkanda mzima upo mikononi mwa Amani.
Tukio hilo limetokea july 15 wakati Bw Said na mama huyo(mama ALI) wakiwa ndani ya nyumba ya Ali iliypo kijijini humo.
MWENYE MKE ATIBUKA NA MAJIBU, AMWAGA DAMU Jibu hilo lilidaiwa
kumtibua Ali na ndipo yeye na baunsa wake wapomfunga kamba miguuni Said
na kuanza kumkata kwa panga mguu mmoja kisha kuugeukia wa pili. Said
alipiga mayowe yaliyowafanya wanakijiji kukimbilia eneo la tukio kwa
lengo la kujua kulikoni ambapo walimkuta Said akiwa anavuja damu na
sehemu ya nyuma ya miguu ikiwa nyanganyanga.
MWENYE MKE AKIMBIA, ANASWA Ali, God na
baunsa walikimbia eneo hilo. Baadhi ya wanawake walitumia khanga zao
kuifunga miguu ya Said kwa lengo la kujaribu kuzuia damu isiendelee
kumwagika. Said alikuwa akilia sana.Wanakijiji walichukizwa sana
na ukatili uliofanywa na Ali, hivyo wakaanza kumsaka na kumkamata
kichakani akiwa amejificha pamoja na God. Alipewa mkongoto kwa lengo la
kutaka kumuua, lakini viongozi wa kijiji walisihi asiuawe bali
afikishwe kwenye kituo cha polisi, alisema shuhuda.`
GPL
No comments:
Post a Comment