SAFARI YANGU YA KWENDA TABORA.
S
|
Nimetumia siku tano so nitakuwa naielezea kwa day after day ila briefly ili iwe rahisi kujua yote toka naenda mpaka narudi.
I
|
la wakati naipanga hii safari ili kwenda kumuona mume wangu, iliniweka katika wakati na maamuzi magumu sana kama fans zangu mnavyofahamu nina watoto wadogo akiwepo mdogo wa miezi mine 4, Tabora ni mbali sana ni mwendo wa karibia masaa 14 kutokea Dar Es Salaam watoto ni wadogo nikisafiri nao nikaona nitakuwa nawatesa, Nikafanya maamuzi magumu mno ya kuwaacha wanangu kwa wadada wasaidizi wangu wa nyumbani. Hizi ni changamoto za maisha inapofika wakati mgumu kama huu ulionifikia mimi inabidi ufanye maamuzi mazito, so nikawaacha wanagu Lincon na Linstone.
Si mabali kutokea pale Tabora Mjini ni kama mwendo wa Dk 5
hivi kwa Gari, tukawa tumefika gerezani pale, Tukaelekezwa taratibu za kufuata kujiandikisha na kila kitu halafu tukaambiwa tusubiri kwa zamu yetu mana pia tulikuta watu wengine ambao nao walikuwepo pale kuwaona ndugu jamaa na marafiki zao. Muda wetu ulipofika na sie tukaitwa katika listi tukapelekwa huko gerezani, hapo mapokezi kuna sheria zao za kuzima simu na kuacha kila kitu so baada ya kuacha tukaingia katika hiko kijichumba kidogo tu.
K |
iukweli it was a very SAD moment, nilipomuana mume wangu, akiwa kwa upande wa pili na sikuwa namuona vizuri mana hiyo nyavu iliyotenganisha hapo ilikuwa kuu kuu, Nilishindwa Kujizui MACHOZI yalianza kunitoka, Ila mume wangu alikuwa MORE THAN STRONG akinisihi nisilie ye yuko poa, Kiukweli Kauli hii ilinipa nguvu, nikashangaa na mie Napata nguvu. Swali la Kwanza aliniuliza Vipi WATOTO hawajambo? Umekuja Nao? Nikamjibu wako wako salama , Kutokana na umbali wa safari nimeonelea nisije nao”Hapa Pia Naendelea Kuamini Kuwa MUNGU bado Yuko Upande Wetu, Misukosuko niliyoipata njiani nawaza ningekuwa na watoto ingekuwaje”?? .Tukaongea mawili matatu kama dakika tano hivi tukaambiwa muda umekwisha tunatakiwa kutoka. Kuna nguo nilibeba tukaambiwa zikakaguliwe kwanza then ndo atakabidhiwa tukafanya kama maelezo yalivyotaka then tukaondoka.
K
|
iukweli after kumuona mume wangu hapo ndo nikawa na uhakika wa aslimia mia kuwa yuko mahali Fulani nikarudi zangu hoteli, ila nilipata mda mchache sana na nilikuwa na maswali kibao, tukaulizia taratibu za pale wakatuambia kwa waliotoka mbali huwa wanapata nafasi siku za kazi kwa at least hata dk kumi, so nikipanga kurudi tena siku ya Jumatatu.
Jioni Baada ya Kutoka Gerezani, Nilikutana na Sister Wangu ambaye hatujaonana zaidi ya miaka 20. Kwenye post ya changamoto na opportunity nae mtamfahamu.
DAY4.JUMATATU
N
|
iliamka asubuhi na kujiandaa, Baada ya kumaliza nikatoka kwenda kutafuta baadhi ya vitu alivyoniagiza, So nilipokamilisha vyote nikaanza safari ya kwenda Gereza Kuu Uyui kwa siku nyingine tena, Leo nikiwa nimeongozana na mwanasheria ambaye yeye anafanya shughuli zake kule kule kwa ajili ya mambo mawili matatu.
T
|
Nikiwa na mwanasheria.
T
|
Hapa Nikiagana na Mwanasheria.
DAY5.JUMANNE
B
|
aada ya kukosa usafiri wa kurudi Dar Siku ya Jumanne, nikitazama Tabora ni mbali nikasema ngoja niende Gerezani kuomba hata dakika moja ya kumuaga mume wangu, nikaelekea gerezani Uyui, Ila dah nikaomba sana wanilikatalia, nikaamua kurudi zangu kiunyonge hotelini, kuja kusubiria Jumatano kusafiri kurudi zangu Dar.
DAY6.JUMATANO
N
|
ikaanza safari ya kurudi dar, Tuliondoka Tabora saa 12 asubuhi, After Masaa Mengi njiani by saa 2 na nusu hivi nikafika salama Dar, nilikuwa So excited kuwaona wangu, Thanx God Nilifika salama na niliwakuta wanangu wako salama.
NYONGEZA
Jumatatu tarehe 8/Julai/2013, mume wangu anapandishwa tena mahakamani huko Tabora, Bado nahitaji msaada wenu katika kunisaidia maombi.
SHUKRANI.
N
|
apenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wote wote ambao mpaka sasa mko pamoja na familia yangu, Kiukweli ni wengi mno sitaweza kuwataja wote na naomba msinihukumu kwa hilo ni wengi mno, Ila kwanza kabisa naendelea kumshukuru Mungu naamini yuko pamoja na familia yangu, naamini hatatuacha , pili kwa wasaidizi wangu wa kazi nyumbani kwangu niliwaachia wanangu mikononi mwao na nikawakuta wako salama, Ndugu wote wanaonisupport, marafiki wote wanaonisupport, Ila Shukrani zangu za dhati pia ziwaendee FANS wangu woteeeeee popote walipo kwa kunisaidia kwenu katika maombi inatia moyo
Source. www.joycekiria.com
No comments:
Post a Comment