Baada Waziri wa Ujenzi, Pombe Magufuli kutoa maagizo kwa wenye majengo yaliyo pembezoni mwa barabara ya Ali Hassan Mwinyi, kubomoa wenyewe majengo yao ili kupisha upanuzi wa barabara hiyo, kuonekana yakisua sua, hatimaye leo ameanza rasmi kazi ya kubomoa kwa Greda katika majengo ya wale walioonekana kukaidi agizo hilo.
Katika kutekeleza agizo hilo zoezi hilo limeanzia kwenye Jengo la Business Park (Green Acres) lililopo eneo la Victoria ambapo hadi hivi sasa zoezi hilo bado linaendelea pande hizo chini ya usimamizi ya Askari
Msongamano pande hizo.....
Tayari ukuta ukiwa umeshashushwa chini wa upande wa barabarani huku baadhi ya watu wanaofanya shughuli zao katika jengo hilo wakihaha kuhamisha baadhi ya vifaa.
Katapila likiendelea na kazi ya kubomoa hapa ni jengo la pili lililokaribu na Green Acres nalo likiliwa hapa tayari ukuta ukiwa unashushwa.....
Sufianmafoto
No comments:
Post a Comment