Tuesday, 4 June 2013

PAMOJA NA KUTUMIKIA KIFUNGO CHA NJE, SHEIKH PONDA ASEMA MIHADHARA ITAENDELEA KAMA KAWA!



https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhx6Q448Tk_h6F9iPgHRccgvOvOjxhCSIbDAN8HggoIlIovCqKMdK694MpNMGSDgu3fTCo0r05VQJ_Yh_Ks84_RBxZFq9g3dB2WlKMZcfQwwhlKOgy-Jz0qXIuUTKluO3XHFxUgvHS53LFf/s640/DSC_0304.JPGKATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, ameibuka na kutangaza kuendeleza mihadhara iliyokatazwa na kupigwa marufuku na serikali.

Mbali na kutangaza hayo pia amesema watapigania kurudishwa kwa mitihani ya dini ambayo serikali imefuta mitihani hiyo.
 
Hayo ameyasema juzi katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam kwenye kongamano la kujadili mada mbalimbali yakiwemo ya mambo yawahusuyo Waislamu nchini

Wakati akitangaza hayo alimtaka Waziri wa Mambo ya Ndani azingatie kauli hiyo kwani ni muhimu waendeleze na kudai hiyo si haki na hiyo ni sawa na kukubali ujinga.

Hivyo alisema mihadhara hiyo itaendelea kama kawaida na atakayejitokeza kukataza mihadahara hiyo watakabiliana nae kwa nguvu zote,” alisema Ponda.

Pia sakata la kufutwa kwa mitihani ya masomo ya dini limeonekena kuwa utata katika kongamano hilo kwani imeonekana kitendo hicho ni kufanya wanafunzi kukosa moyo kujifunza masomo hayo
Hilo limekuja baada ya serikali kufuta mitihani ya masomo ya dini na kuhakikisha kujifunza pekee mashuleni
Hivyo waislamu hao wamesema watahakikisha mitihani hiyo itarudisha kama kawaida kwani wameona kitendo hicho ni kuua elimu ya dini kwa watoto wa kiislamu

Shekhe hivi sasa anatumikia kifungo cha nje alichohukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatia kupatikana na makosa ya uchochezi

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!