Chande Abdallah na Denis Mtima
Tafadhalini msaada wadau! Mtoto Hamis Hashim Bakari, mwenye umri wa miaka 13, anapata mateso makubwa akisumbuliwa na tatizo la miguu kujaa maji kutokana na kugundulika kuwa na mifupa laini tangu mwaka 2008.
Mtoto Hamis anaishi na wazazi wake Yombo Dovya, jijini Dar. Tatizo lake lilianza alipovunjika mguu wa kushoto ambao ulijaa maji na kuvimba.
Katika harakati za kupata matibabu, Hamis alitibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya
kugundulika tatizo na akawa ameshindwa kutembea huu mwaka wa tano sasa.
Muda wote Hamis anatambaa kutoka sehemu moja kwenda nyingine huku safari ndefu akizifanya kwa msaada wa Baiskeli aliypewa na shule ya msingi Yombo dovya.
Mtoto Hamisi anaomba msaada kwa wasamaria wema ili aweze kupata matibabu.
KWA YEYOTE ALIYEGUSWA NA HABARI HII WASILIANA NA SIMU HII 0714452275.
k
kwa msaada wa…
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment