Tunahabarishwa kuwa hali ni mbaya huko Mtwara. mabomu ya machozi yanarindima muda huu na huduma zote za kijamii zimefunngwa hakuna usafiri, masoko, maduka n.k
Habari hizo zimeongeza kuwa Daraja la Mikindani limevunjwa na hakuna mawasiliano Mtwara na Dar es salaam.
Kwa mujibu wa habari zisizo na uthibitisho, baadhi ya Wananchi wamepora Silaha na wanazitumia kujibu mashambulizi ya Jeshi la Polisi
Kwa ujumla kinachoendelea ni mapambano makali kati ya Jeshi la polisi na wananchi wenye hasira wanaopinga vikali kuendelea kwa mchakato wa gesi ilihali nchi ikiwa haina sera inayosimamia nishati hiyo.
Kufuatia Kambi ya Upinzani kuukataa mpango wa serikali wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara Mpaka Dar es salaam.
Jengo la Ofisi ya CCM saba saba limechomwa moto.
Lodge/Hotel (Shengena) inayoaminika kwamba ndiyo waliyofikia Askari wa Jeshi la Polisi (FFU) kutoka mikoa ya jirani kwaajili ya operation inayoendelea imechomwa moto.
Milio ya risasi na mabomu ndicho kinachosikika.
Nyumba kadhaa za watumishi wa Serikali zimechomwa maeneo ya Shangani
Ni magari ya FFU ndio yaliyopo barabarani nayo yanapata wakati mgumu kupita kwasababu ya mawe na magogo makubwa yaliyowekwa na Wananchi.
.
Habari kwa hisani ya mpekuzi
No comments:
Post a Comment