skip to main |
skip to sidebar
TAHADHARI
Tangazo Muhimu Kwa Umma Kutoka Benki Kuu ya Tanzania.
Benki Kuu inapenda kuutahadharisha umma kuwa katika siku za karibuni kumekuwepona mtandao wa matapeli unaotumia TOVUTI ifuatayowww.jakayafoundation.wapka.mobi/index.html.Mtandao huo unajidai kuwa ni Taasisi ya Fedha ijulikanayo kwa jina la Jakaya foundation ambayo inamilikiwa na Benki Kuu chini ya utawala wa bodi kuu ya mikopo inayotolewa na serikali kupitia sekretariat ya Utumishi wa umma ofisi ya Rais.
Matapeli hao wanaeleza kwamba Taasisi hiyo inatoa mikopo ndani ya masaa 24 kwa Mtanzania yeyote mwenye umri kuanzia miaka 18 endapo atajiunga kwa kulip a ada ya shilingi 37,000/=.BENKI KUU INAUARIFU UMMA KUWA HAIITAMBUI NA WALA HAIHUSIANI KWA NAMNA YOYOTE ILE NA TAASISI INAYOELEZWA KWENYE TOVUTI HIYO.
Kwa taarifa hii, Benki Kuu inatoa tahadhari kwa Wananchi kutojihusisha na Taasisi hiyo ya kitapeli kwa ajili ya kupata huduma za mikopo kama ambavyo inadai.
IMETOLEWA NAIDARA YA UHUSIANO NA ITIFAKIBENKI KUUYA TANZANIADAR ES SALAAM.29/5/2013
No comments:
Post a Comment