Friday 17 May 2013

MAJAMBAZI YAVAMIA BAR NA KUMCHINJA MLIZI JIJINI DAR-ES-SALAAM. HALI INATISHA KWA KWELI....

Mlinzi wa baa ya Darajani Stop Over iliyo kando kando ya barabara kuu ya Morogoro Dar es salaam jirani na daraja la Mzambarauni  Bw Mika Athumani amechinjwa na majambazi usiku wa kuamkia leo.


Habari zilizopatikana eneo la tukio zilidai kwamba majambazi hayo yalivamia baa hiyo iliyojitenga usiku wa manane na kumvamia mlinzi huyo na kumchinka kama kuku na baadae kuvunja baa hiyo na kuiba vitu mbali mbali.

Mwili wa marehemu ukiwa ndani ya gari, la polisi kufuatia mwili huo kutenganiswa vibande viwili..
Sehemu aliyochinjiwa mlinzi huyo aliyefahamika kwa jina Mika Athumani

Majira ya saa 12 asubuhi ya leo wananchi walishuhudia maduka mawili ya baa hiyo yakiwa wazi huku mwili wa mlizni huyo umekutwa upande wa baa ukiwa umechinjwa na kutenganishwa kichwa na mwili
Mmiliki wa baa hiyo Bw Salvatory Mushi alidai kwamba majambazi hao walimvamia mlinzi wake na kumchinja na baadae walivunja Counter ya baa hiyo pamoja na duka ililipojirani na baa hiyo na kuiba vitu mbali mbali.
 

Alipoulizwa kwamba kuna taarifa zinadai kwamba mlinzi huyo alikutwa akiwa amelala Bw Mushi alisema"  inawezekana lakini hakuna mtu mwenye uhakika na jambo hilo kwani sote hatukuwepo,wakati tukio hilo linatokea.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!