Baada ya Mahojiano Rama alikiri kuwa alikuwa na tabia ya kula nyama za watu na kwamba ni tabia ambayo amefundishwa kichawi toka alipokuwa mdogo. Mahakama imemuachia huru kwasababu mtuhumiwa alitenda kosa hilo pasipo kuwa na akili timamu. Hata hivyo mahakama hiyo imetoa agizo la kuendelea kumuweka kijana huyo katika hospitali ya wagonjwa wenye matatizo ya akili iliyopo Dodoma. k mama wa Kijana huyo (Bi Khadija Ally) ambaye pia alikuwa rumande kufuatia tuhuma hizo, aliachiwa huru. Rama amepelekwa hospitali ya Isanga iliyopo Dodoma mpaka pale atakapona.
![](http://2.bp.blogspot.com/-qcVgOHNRAzw/UZ9kvpCmz4I/AAAAAAAAnjA/E0w__7Gus40/s1600/RAMAMLAVICHWA4.jpg)
Ramadhani akiwa na mama yake mzazi, Khadija Ally wakielekea mahakamani.
Kijana Ramadhani akihojiwa.
Mama wa Marehemu Salome akilia kwa uchungu wakati wa mazishi ya mwanae.
Kijana Ramadhani akiwa na mama yake mzazi.
No comments:
Post a Comment