Mlipuko mkubwa umetokea katika kanisa Katoliki la Mt Joseph Mfanyakazi Parokia ya Olasisi Arusha. Watu kadhaa wamepoteza maisha, na wengine wamejeruhiwa vibaya, mlipuko huo umetokea wakati wa ibada ya uzinduzi wa kanisa hilo iliyokuwa ikiongozwa na Balozi wa Papa nchini. Endelea kutufuatilia kwa taarifa zaidi, na kwa habari za kuaminika tulizozipata zinasema mtu mmoja amefariki dunia na wengine 49 kujeruhiwa vibaya, katika mlipuko huo ambapo unasadikiwa kuwa ni kitu kama Bomu. Tukio hilo limetokea leo majira ya saa 4 asubuhi, wakati wa sherehe za ufunguzi wa kanisa la Mt. Joseph la Roman katolik, lililopo Olasiti jiji Arusha.
Majeruhi akipata huduma ya kwanza
Eneo hilo lililozungushiwa utepe ndio sehemu inayodhaniwa kuwa bomu hilo lilitua.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo akizungumza na mmoja wa mapadri wa Kanisa hilo kupewa maelezo ya kuhusu kilichotokea kanisani hapo.
Viongozi wa Kanisa wakitoa taarifa ya kilichotokea kwa waandishi wa habari kabla ya Balozi wa Papa kuondolewa Kanisani hapo chini ya ulinzi mkali wa Polisi
No comments:
Post a Comment