Pages

Tuesday 7 May 2013

JINSI YA KUEPUKA NA UGONJWA WA( CANCER) SARATANI....



zaidi ya nusu ya vifo vinavyotokana na magonjwa ya Saratani vinaweza kuzuiwa kwa kufanya maamuzi sahihi ya kiafya kama vile, kuacha kuvuta sigara, kuwa nauzito wa mwili unaokubalika kiafya, kula vyakula sahihhi, kufanya mazoezi, na kufanya vipimo vya kucheki afya mara kwa mara kama inavyoshauriwa.



Nukuu kutoka chama cha wagonjwa wa saratani nchini Marekani, nukuu ambayo inatakiwa kuchukuliwa kwa uzito mkubwa sana nakutambua kwamba jukumu la kujiepusha na magonjwa ya saratani linaanza na wewe..
ZIFUATAZO NI NJIA ZA KUZUIA MTU KUPATA MAGONJWA YA SARATANI ENDAPO ATAZINGATIA HAYA:
.
KUWA NA VITAMIN D.
Hakikisha unaota jua ili kupata kiwango cha kutosha cha  kutosha cha Vitamin D, kama huna nafasi ya kupata mwanga wa jua tumia vidonge D3. Imethibitishwa na wanasayansi kuwa mwili ukiwa na Vitamin D ya kutosha unajiepusha na uwezekano wa magonjwa ya Saratani.

ULAJI WA PROTINI ULIOKITHIRI.
Baadhi yetu tunakiwango kikubwa cha protini mwilini kutokana na kupenda kula vyakula kama vile nyama. Tunashauriwa kula nyama au vyakula vingine vinavyoongeza protini kwa siku isizidi kiwango cha gram 100. Inaruhusiwa kuzidi kiwango hicho kwa kina mama wajawazito, na watu wenye kufanya mazoezi ya kukimbia kwa umbali mrefu.

VYOMBO VYA KUPIKIA.
Hakikisha unatumia vyombo vya kupikia ambavyo vimeoshwa vizuri, kwa kutumia sabuni ya kawaida na maji safi, usipende kuosha vyombo vyako kwa kutumia sabuni au dawa yenye kemikali nyingi, kwani baadhi ya kemikali huleta saratani.

BIDHAA ZA NGOZI.
Kuna aina nyingi sana za bidhaa za ngozi, lakini baadhi ya bidhaa hizo kama vile lotion, krimu, mafuta  n.k zimetengenezwa kutokana na kemikali ambazo zinaaminika kusababisha saratani ya ngozi. Unashauriwa kujiepusha na bidhaa hizo, na badala yake tumia bidhaa zilizotengenezwa kutokana na mimea,au matunda asilia.



Hakikisha unakunya maji kila siku yaliyo safi na salama, yaliyohifadhiwa katika chombo safi na kuwekewa dawa ya kusafisha maji inayokubalika.

VYAKULA VYA MADAWA.
Jiepushe kula vyakula kama vile mboga, matunda, na  mimea mingine ilyooteshwa na kustawishwa kwa kutumia madawa ya kunenepesha mimea hiyo(GMO) badala kula chakula, vilivyolimwa na kustawishwa kwa kutumia udongo na mbolea asilia(ORGANIC FOOD)

VYAKULA VYA MAKOPO.
Epuka kutumia vyakula vya makopo vinavyotengenezwa na kuhifadhiwa. Kemikali zinazotumika katika utengenezaji wa makopo hayo ili yaweze kuhifadhi chakula na kikae kwa muda mrefu, zinadaiwa kusababisha kansa, ili kuwa salama zaidi jiepushe na ulaji wa vyakula vyote vya makopo.

ZINGATIA.
Kula mboga za majani, nyanya, brokoli, kabichi, matunda kwa wingi kama vile nanasi, stafeli, fenesi, komamanga, maeple an mengine mengi, ukiwa na tabia ya kula matunda mara kwa mara, unauhakika wa kinga imara ya mwili, si saratani tu bali kwa magonjwa yote hatari.




imetolewa na Glob Publishers..

No comments:

Post a Comment