Tuesday 21 May 2013

Diwani wa Mswaha, wilayani Korogwe afanya shughuli za utoaji majini wilayani Muheza .... Mambo haya

Mganga wa jadi Aweso Kipaku ambaye ni diwani wa kata ya Mswaha iliyopo wilayani Korogwe, akiwa ameshikilia kitu kinachodaiwa ni jini alilolitoa katika moja ya darasa la shule ya msingi Kwemsala iliyopo kata ya Mtindiro wilayani Muheza juzi, wengine aliyevaa fulana ya punda milia ni mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Shabani Hamisi.
                                                                              ******
Na Mashaka Mhando, Muheza
LICHA ya serikali mkoani Tanga kusikika ikipiga marufuku masuala ya utoaji uchawi katika sehemu mbalimbali za wilaya zake mkoani humo, lakini diwani wa Kata ya Mswaha, iliyopo wilayani Korogwe, Aweso Kipaku ambaye pia ni mganga aliendeleza shughuli hizo katika kijiji cha Kwemsala, wilayani Muheza mkoani Tanga, kwa madai kuwa shule ya kijiji hicho ilikuwa na imani za ushirikina. 

Akifanya kazi hiyo, juzi katika shule hiyo Diwani huyo aliyealikwa na kamati ya shule ya kijiji hicho, alianza kupita kila darasa la shule hiyo huku akionekana amepandisha mapepo yaliyokuwa yakimuongoza huku wananchi wa kijiji hicho wakijazana kuona kazi anayofanya diwani huyo.

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!