Pages

Monday 20 May 2013

15 MBARONI KWA KUCHOMA MAKANISA MAWILI HUKO TANGA








Polisi  mkoani Tanga inawashikilia watuhumiwa 15, wanaodaiwa kuchoma moto Kanisa la Bethania lililoko eneo la Donge  Mkoani humo , siku ya ijumaa iliyopita usiku.
 
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Costantine Massawe, alisema watuhumiwa hao walikamatwa usiku huo huo katika maeneo tofauti ya mji wa Tanga.


Kwa mujibu wa Kamanda Massawe, Polisi pia inachunguza tukio jingine la kutaka kuchoma moto Kanisa la Miracle Revival, lililoko katika mji wa Makorola

Usiku wa kuamkia juzi, watu wasiojulikana walijaribu na kuchoma moto makanisa mawili, banda moja la kuoneshea picha za video na banda la pombe za kienyeji, na kusababisha hofu ya uhalifu dhidi ya dini ya Kikristo kuenea miongoni mwa wakazi mkoani hapa.


 Kanisa la Betham lililokuwa likitumika zamani, liliteketezwa kwa moto na baada ya hapo watuhumiwa waliingia ndani ya kanisa kubwa la sasa, na kuchoma moto vitambaa vilivyofunika madhabahu.
Aidha imefahamika kuwa, Kanisa la Miracle Revival lililopo eneo la Makorola, lilinusurika kuchomwa moto baada ya  juhudi hizo kuzimwa na watu waliojitolea kuuzima, wakati ulipokuwa umeshawashwa kwenye nguzo za kanisa hilo.


No comments:

Post a Comment