Polisi mkoani Tanga inawashikilia watuhumiwa 15, wanaodaiwa kuchoma moto Kanisa la Bethania lililoko eneo la Donge Mkoani humo , siku ya ijumaa iliyopita usiku.
Kwa mujibu wa Kamanda Massawe, Polisi pia inachunguza tukio jingine la kutaka kuchoma moto Kanisa la Miracle Revival, lililoko katika mji wa Makorola
Usiku wa kuamkia juzi, watu wasiojulikana walijaribu na kuchoma moto makanisa mawili, banda moja la kuoneshea picha za video na banda la pombe za kienyeji, na kusababisha hofu ya uhalifu dhidi ya dini ya Kikristo kuenea miongoni mwa wakazi mkoani hapa.
Kanisa la Betham lililokuwa likitumika zamani, liliteketezwa kwa moto na baada ya hapo watuhumiwa waliingia ndani ya kanisa kubwa la sasa, na kuchoma moto vitambaa vilivyofunika madhabahu.
Aidha imefahamika kuwa, Kanisa la Miracle Revival lililopo eneo la Makorola, lilinusurika kuchomwa moto baada ya juhudi hizo kuzimwa na watu waliojitolea kuuzima, wakati ulipokuwa umeshawashwa kwenye nguzo za kanisa hilo.
No comments:
Post a Comment