Friday 26 April 2013

UPENDO, UMOJA, UTULIVU, AMANI NA MSHIKAMANO HIZO NI SALAMU KUTOKA UK KATIKA KUSHEREHEKEA MIAKA 49 YA MUUNGANO WA TANZANIA .




Tawi la chama cha mapinduzi nchini Uingereza limetoa salamu kwa aidha kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dr.Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed  Shein, kwa  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,na  kwa WaTanzania wote kwa ujumla kwa kutimiza miaka 49 ya Muungano wa nchi yetu, TANZANIA.

Aidha chama hicho kimewasihi watanzania kuendelea kuulinda Muungano wetu kwa kudumisha AMANI, UPENDO, UMOJA, UTULIVU na MSHIKAMANO, kwani hizo ndizo silaha zilizoweza kuulinda Muungano huu ambao umetuletea Heshima ya kipekee Duniani kote, kwa nusu karne sasa.

Katika salamu hizo wana CCM nchini Uk wamesisitiza kuwa tujifunze kutoka nchi mbalimbali duniani ambazo wamechezea amani yao na sasa wamo ndani ya dimbwi kubwa la machafuko, mauaji ya halaiki na yanayoendelea kila kukicha.  Maelfu ya raia wasio na hatia wamepoteza maisha yao katika Nchi mbalimbali, wengine kupata ulemavu wa kudumu, kupoteza makazi na kuharibikiwa na mwenendo mzima wa mfumo wa maisha yao, milipuko ya mabomu isiyoisha na raia kukosa amani na utulivu. WaTanzania kamwe tusikubali kuipoteza amani yetu kwa uchochezi wa watu wachache, na ambao kwa sababu zao binafsi  hawatutakii  mema , na mpaka wako tayari kutumia  visingizio kama vya siasa na dini ili watusambaratishe.

CCM UK, pia imetoa shukrani za dhati kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete , pamoja na Serikali yake anayoiongoza kwa kuona umuhimu wa  WanaDiaspora na kuthamini mchango wao na kwamba,wataendelea kuchangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya Tanzania kama inavyowezekana kwa raia wengine   wengi waishio  nje ya Nchi zao na wanachangia kukuza uchumi na kuendeleza jamii zao kwa kutumia ujuzi na ufanisi waliojifunza ughaibuni.




habari kwa hisani ya
Mariam A. Mungula
KATIBU
CHAMA CHA MAPINDUZI – UINGEREZA

 

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!