Saturday 27 April 2013

RAIS JAKAYA KIKWETE ATOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA ZAIDI YA 4000.



 Rais Jakaya Kikwete ametoa msamaha kwa wafungwa 4,180 waliokuwa wakitumikia vifungo vyao katika magereza mbalimbali hapa nchini.
Msamaha huo ulitolewa wakati wa sherehe za kuadhimisha miaka 49 ya muungano wa Tanzania.
 
Wafungwa waliosamehewa ni wanaotumikia kifungo kisichozidi miaka mitano, ambapo mpaka siku ya msamaha yaani April 26, watakuwa wameshatumikia robo ya vifungo vyao, wafungwa wagonjwa wa Ukimwi, kifua kikuu na kansa ambao wamethibitishwa na jopo la madaktari.
 
Pia wazee wenye umri wa miaka sabini au zaidi, wafungwa wa kike walioingia na mimba gerezani, walioingia na watoto wanaonyonya na wasionyonya, wakiwamo walemavu.
 
Msamaha wa Rais pia umeenda kwa wafungwa walemavu wa mwili na akili na wafungwa ambao hadi siku ya jana walikuwa wameshakaa gerezani kwa muda wa miaka mitano na wameonyesha kuwa na tabia nzuri

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!