Lengo la uzinduzi wa mpango huu ni kuandaa mazingira mazuri ya kisera, sheria, mikakati na miongozo kuhusu upatikanaji wa haki za watoto hapa nchini ikiwemo kuzuia vitendo vya ukatili dhidi yao, mpango utakaotekelezwa kati ya mwaka 2013 hadi 2016.
Uzinduzi wa mpango huu unatarajiwa kufunguliwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Mhe. Jenista Mhagama (Mb), utakaofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Dodoma, mkoani Dodoma siku ya Ijumaa ya tarehe 12 Aprili 2013, saa 7:00 mchana
No comments:
Post a Comment