![](https://fbcdn-sphotos-h-a.akamaihd.net/hphotos-ak-prn1/155517_109266299145881_7899190_n.jpg)
MWIMBAJI ambaye pia ni bosi wa Kundi la Mashauzi Classic, Aisha Ramadhan Makongo ‘Mashauzi’, Jumatano iliyopita alikumbwa na mkasa mzito kufuatia kudakwa na polisi wa Kituo cha Msimbazi jijini, kwa tuhuma za kukwapua mkoba wenye kitita cha shilingi laki saba, elfu hamsini na nane na mia mbili (758,200) mali ya Veronica Tarik.
Chanzo cha habari kituoni hapo kilidai kuwa Jumanne iliyopita, Isha Mashauzi na shosti wake aliyejulikana kwa jina la Halima Shaban waliingia duka moja Mtaa wa Mafia na Jangwani, Kariakoo, Dar kwa lengo la kufanya ‘shopping’ lakini walipochomoka, Veronica alishangaa kutouona mkoba wake, na ndipo alipoamua kuwafuata vichuna hao, na kwamba waligoma kusachiwa na muhusika, tendo ambalo lilipelekea tajiri huyo kuripoti polisi, na kuwafungulia mashitaka.
Isha akiwa selo, wapambe wake walimiminika kituoni hapo akiwemo Mtangazaji wa Kituo cha Redio Times FM cha jijini Dar, Hadija Shaibu ‘Dida’ kwa ajili ya kuhangaikia kuwachomoa wawili hao
Washitakiwa walitolewa kwa dhamana.
Habari kwa hisani ya mpekuzi.
No comments:
Post a Comment