Sunday 28 April 2013

JAMANI MNAAMBIWA KILA MTU ANA WIVU, TOFAUTI NI AINA YA WIVU, SOMA HIYO UJUWE WIVU WAKO NI UPI?

KILA MTU ANA WIVU!!!!!!!!
KILA M2 ANA WIVU!!!!!!!!!
Kila mtu duniani ana chembechembe za wivu! Tunachotofautiana ni kiwango cha wivu na masuala tunayoyaonea wivu. Wapo ambao chembechembe za wivu zimewaenea mwili mzima kiasi kwamba hujisikia vibaya hata wenza wao wakishikana mikono na wengine! Hawa huvizia simu za wapenzi wao na kupekua kutazama wanawasiliana na kina nani!

Upo pia wivu wa kawaida. Wenzetu wanapopata mafanikio kwenye nyanja mbalimbali, chembechembe za wivu huanza kuchemka mwilini na kutamani mafanikio yao yangekuwa yetu. Wivu huu huwa na maana kama unatupa mshawasha na kutushajiisha kujituma ili kuyafikia mafanikio tuyatamaniyo!

Wivu mbaya ni ule unaoambatana na chuki na ‘’roho ya kwa nini’’. Chembechembe za wivu wa namna hii zikimuingia mtu mwilini anaweza kuchukua uamuzi mbaya unaoweza kumduwaza hata shetani! Hujawahi kusikia watu wakijiua ama kuua wengine kinyama kwa sababu ya wivu?

Mara nyingi chembechembe za wivu hutuingia mwilini bila hata wenyewe kujua. Kuhusu hili la kila mtu kuwa na ‘’maradhi’’ ya wivu kidogo, Okot P’ Bitek, malenga mashuhuri wa Uganda anatuambia;

…I do not deny
I am a little jealous.
It is no good lying,
We all suffer from a little jealousy.
It catches you unawares
Like the ghosts that bring fevers;
It surprises people
Like earth tremors…

Kila mtu duniani ana chembechembe za wivu! Tunachotofautiana ni kiwango cha wivu na masuala tunayoyaonea wivu. Wapo ambao chembechembe... za wivu zimewaenea mwili mzima kiasi kwamba hujisikia vibaya hata wenza wao wakishikana mikono na wengine! Hawa huvizia simu za wapenzi wao na kupekua kutazama wanawasiliana na kina nani!

Upo pia wivu wa kawaida. Wenzetu wanapopata mafanikio kwenye nyanja mbalimbali, chembechembe za wivu huanza kuchemka mwilini na kutamani mafanikio yao yangekuwa yetu. Wivu huu huwa na maana kama unatupa mshawasha na kutushajiisha kujituma ili kuyafikia mafanikio tuyatamaniyo!

Wivu mbaya ni ule unaoambatana na chuki na ‘’roho ya kwa nini’’. Chembechembe za wivu wa namna hii zikimuingia mtu mwilini anaweza kuchukua uamuzi mbaya unaoweza kumduwaza hata shetani! Hujawahi kusikia watu wakijiua ama kuua wengine kinyama kwa sababu ya wivu?

Mara nyingi chembechembe za wivu hutuingia mwilini bila hata wenyewe kujua. Kuhusu hili la kila mtu kuwa na ‘’maradhi’’ ya wivu kidogo, Okot P’ Bitek, malenga mashuhuri wa Uganda anatuambia;

…I do not deny
I am a little jealous.
It is no good lying,
We all suffer from a little jealousy.
It catches you unawares
Like the ghosts that bring fevers;
It surprises people
Like earth tremors

No comments:

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!