Pages

Wednesday, 9 October 2024

Rubani afariki akiwa angani

Rubani wa shirika la ndege la Uturuki amefariki dunia akiwa katikati ya safari

-Ndege hiyo aina ya Airbus A350-900 iliyokuwa ikitokea Seattle nchini Marekani kuelekea mji mkuu wa Uturuki Istanbul, ililazimika kutua kwa dharura New York baada ya rubani huyo kufariki.

-
Rubani huyo mwenye umri wa miaka 59, Ilcehin Pehlivan, "alizimia" wakati wa safari hiyo ya ndege.
-
"Baada ya kujaribu kutoa huduma ya kwanza, wafanyakazi wa ndege na rubani mwena waliamua kutua kwa dharura, lakini alifariki kabla ya kutua,"
-
Rubani huyo amefanya kazi na Shirika la Ndege la Uturuki tangu mwaka 2007.

BBC.

No comments:

Post a Comment