Pages

Saturday, 11 February 2023

AKA AFARIKI

 Baadhi ya Mitandao ya Afrika Kusini ukiwemo Mtandao wa TimesLIVE na iol imeripoti kuwa Rapper maarufu nchini humo Kiernan Jarryd Forbes maarufu kama AKA, amefariki kwa kupigwa risasi akiwa Jijini Durban alikokua amekwenda kikazi.


Japokuwa taarifa hizi bado hazijathibitishwa rasmi na Mamlaka za Durban, Watu maarufu mbalimbali wa South Africa akiwemo DJ Black Coffee, Mtangazaji TBO Touch na Rapper 2FreshLES, bila kutoa maelezo ya ziada wameonesha kuwa katika majonzi kupitia kurasa zao za Twitter usiku huu.
Night Club ya YUGO ya Durban ambayo AKA alitarajiwa kuwepo usiku huu kufanya onesho na kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, imetoa taarifa ya dharura saa mbili zilizopita na kusema tukio hilo limefutwa.
Rapepr AKA amewahi kufanya kazi na Wasanii wa Tanzania ambao ni Diamond Platnumz kwenye wimbo wa "make me sing" ulioachiwa mwaka 2016 na "dont bother" aliofanya na Joh Makini ulioachiwa November 2015. #MillardAyoBREAKING

No comments:

Post a Comment