Pages

Saturday, 4 February 2023

Ajali yaua 17 Tanga wakiwemo ndugu 14 waliokuwa wanakwenda kuzika Moshi

 

Ajali

Watu 17 wamefariki dunia na wengine 12 kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea usiku wa kuamkia leo Jumamosi mkoani Tanga Kaskazini mwa Tanzania.

Inaelezwa katika ajali hiyo inaelezwa watu 14 kati ya 17 waliofariki ni ndugu waliokuwa wakielekea kuzika mwili wa ndugu yao mkoani Kilimanjaro.


Taarifa iliyotolewa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Korogwe, Salma Sued imetaja ndugu waliofariki ni Atanasi Rajabu Mrema, Nestory Atanasi, Augustino Atanasi, Kenned Mrema, Godwin Mrema, Yusuph Saimon, Zawadi Mrema, Elizabeth Mrema, Julieth Mrema, Suzana, Rozina A Lamosa, Evelina Cosmas Mrema na watoto wawili (mtoto wa binamu na mtoto wa Julieth).

Rais Samia Suluhu ameeleza kusikitishwa na ajali ya gari iliyosababisha vifo vya watu 17 mkoani Tanga.

'Nimesikitishwa na vifo vya watu 17 vilivyosababishwa na ajali iliyotokea jana saa 4:30 usiku eneo la Magila Gereza, Wilaya ya Korogwe, Mkoa wa Tanga. Nawapa pole wafiwa na wote walioguswa na vifo hivi. Nawaombea ndugu zetu hawa wapumzike mahali pema na majeruhi wapone haraka', alisema Rais Samia kupitia mtandao wake wa Twitter.

No comments:

Post a Comment