Tuesday, 3 January 2023

Eliza abakwa na kuuawa!

Eliza Mlimbila (17) Mkazi wa Mtaa wa Sigridi uliopo Kata ya Kivavi Halmashauri ya Mji wa Makambako Mkoani Njombe amekutwa amefariki katika Mtaa wa Kahawa baada ya kubakwa, kulawitiwa na kukabwa shingo siku ya mkesha wa mwaka mpya.

Baba mzazi wa Marehemu anayeitwa Meshack Mlimbila amesema Mtoto wake ambaye amehitimu kidato cha nne mwaka jana (2022) alichelewa kurudi nyumbani siku ya jumamosi ya December 31 na alipoulizwa alikuwa wapi aliondoka tena bila kuaga mpaka alipopata taarifa za kifo chake siku ya mwaka mpya.
“Jumamosi tumetoka shambani hatukumkuta nyumbani mpaka saa tatu, aliporudi nikamuuliza lakini alivyotokatoka sikuelewa tena na kwa sababu alikuwa anaweza kutoka na kurudi, mpaka mauti unamkuta sielewi alikuwa wapi,mara kadhaa tumemuonya lakini sijui ni kwa nini haya magenge yake kwasabu unaweza ukamwambia akakuelewa halafu ukakuta tena hayupo”
Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah amehudhuria katika mazishi ya Eliza na kuwahakikishia Wananchi kuwa Wahusika wote watakamatwa huku akiomba waendelee kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu kwao wakati Polisi wakiendelea na uchunguzi.
“Binti amezaliwa mwaka 2005 halafu anafariki kwa kusababishiwa na Mtu haiwezekani, sisi tutafuata taratibu zote kuhakikisha jambo hili tunalishughulikia na wanamakambako muwe na imani jambo la msingi niwaombe tuwe na ushirikiano”

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!