Monday, 1 August 2022

NYUMA YA MAFANIKIO YA MWANAUME KUNA MWANAMKE!

 



Watali walitembelea wanakofugwa mamba ziwani, wakawa katika chombo maalum wakielea nacho kufurahia mamba hao.


Mfugaji mamba akapaza sauti, akisema "atajayejirusha ziwani kuogelea nitampa Dola milioni 10", watalii wote wakawa kimyaaa!

Ghafla, mtalii mmoja mwanaume akarukia majini, akaanza kufurushwa na wale mamba! lakini kwa bahati kubwa aliwahi kujiokoa, hawakufanikiwa kumdhuru. Hule mfugaji akamtangaza kuwa nshindi akisema, "We have a winner!!!", akampa huyo mtalii kitita chake cha dola milioni 10.

Baadaye akiwa kwenye hotelini na mkewe, akamwambia mkewe, "Unajua pale sikuruka mwenyewe, kuna mtu aliyenisukuma!" Mkewe akatabasamu kisha akasema, "mimi ndiye niliyekusuma!".

Kumbe kila kwenye mafanikio ya mwanaume inabidi awe amesukumwa japo kidogo na mwanamke!😀😀

Sorce: Thomas Kawongo

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!