Pages

Wednesday, 1 June 2022

CCTV yanaasa binti akimnyonga Mtoto

 


Mtoto Ericksin Kimaro mwenye umri wa miaka nane amedaiwa kuuawa kwa kunyongwa na msichana wa kazi za ndani kwao Kimara Temboni Jijini Dar es Salaam.


Inadaiwa mfanyakazi huyo wa kazi za ndani alifika kwa mwajiri huyo Jumamosi tarehe 28 May,ameshinda siku ya jumapili na jumatatu mtoto alivyorudi shule mfanyakazi huyo akamnyonga mpaka kufariki Dunia.
Baada ya kutekeleza kitendo hicho,binti alimpigia mama wa mtoto mida ya saa 11:30 jioni na kumweleza mtoto anaumwa na alishindwa kupumua vizuri.Baada ya mama kufika alikuta mtoto ameshakuwa wa baridi kichwani ila kiwiliwili cha moto,baada ya mtoto kukimbizwa Hospital ya Mlonganzila walikuta tayari alishafariki.Shahidi anaeleza kuwa binti huyo alichukuliwa na jeshi la Polisi na bahati nzuri nyumba ilifungwa kamera za ulinzi na walipoangalia walibaini kuwa binti wa kazi ndiye aliyehusika na mauaji hayo.
Inadaiwa kuwa mwajiri huyo alikuwa bado hajamfahamu binti vizuri kwasababu ya kuwa busy na shughuli za kazi.Mama wa mtoto ni Daktari wa Moyo Hospital ya Temeke na baba wa mtoto ni daktari wa wanawake Hospital ya Mlonganzila.

No comments:

Post a Comment