Pages

Tuesday, 6 March 2018

Simulizi

Image may contain: one or more people, people sitting, baby and outdoor
Wanandoa wapya waliooana muda si mrefu,
waliishi maisha ya kimasikini sana.Siku moja
mume akamuita mke wake akamwambia''mke
wangu naondoka naenda safari ya mbali,kwenda
kutafuta mali ili tuje tuishi maisha ya furaha na
raha ila sijui nikiondoka nitakaa huko miaka
mingapi.


Nakuomba mke wangu uwe mwaminifu
usinisaliti na mimi pia huko niendako nitakuwa
mwaminifu sitakusaliti''.Mke alikubali na mume
akaondoka akaanza kutembea.Alitembea kwa siku
nyingi sana hatimaye akafika kwa mkulima mmoja
aliyekuwa anatafuta mtu wa kumsaidia kufanya
kazi katika shamba lake.Yule kijana akaomba kazi
akapata ila akamwambia yule mkulima''nitafanya
kazi ila mshahara wangu utakuwa unanitunzia
mpaka siku nikitaka kuondoka nitakuambia unipe
hizo pesa zangu zote nilizofanya kazi kwako.Yule
mkulima akakubali ombi la yule kijana.Kijana
akafanya ile kazi kwa miaka ishirini,na siku moja
akamwambia boss wake kwamba ataondoka hivyo
ampe pesa zake zote.Yule mkulima akasema
sawa ila nitakupa mambo mawili uchague
moja.Mkulima akasema 1.nikupe pesa zako zote
uondoke au 2.nikupe ushauri wa aina tatu afu
nisikupe pesa zako zote ulizofanya kazi kwangu
kwa kipindi chote cha miaka ishirini.Lakini sitaki
unipe jibu sasa hivi katafakari afu kesho utanipa
jibu umechagua kipi.Yule Jamaa akakaa
akatafakari,kesho yake akaja na jibu.Boss
akauliza unataka kipi?Yule jamaa akasema nipe
huo ushauri wa aina tatu.Boss akarudia tena
''nikikupa huo ushauri ujue sitakupa pesa zako
ulizofanya kazi kwangu.Yule jamaa akasema sawa
ww nipe huo ushauri.Yule Boss mkulima akasema
i.usifanye mambo kimkato na usipende njia za
mkato.
ii.usipende kudadisidadisi na kushangashangaa
mambo yasiyokuhusu mana kuna mambo
mengine ni mabaya ukiyadadisi na kuyashangaa
sana yatakupelekea kifo.
iii.usifanye maamuzi wakati unahasira au
unauchungu.
Baada ya hayo yule Boss akamwambia haya kijana
wangu unaweza kuondoka,shika hii mikate mitatu
hii miwi
li utakula wewe mwenyewe ukiwa njiani
kurudi nyumbani na huu mmoja utakula na mke
wako siku ukifika nyumbani.Jamaa akachukua ile
mikate akaanza safari.Mara akakutana na mzee
mmoja akamwambia''kijana umepitia hii njia?hii
njia ni ndefu sana unaweza kumaliza mwezi
hujafika hivyo pitia hii njia ya mkato utafika
haraka.Jamaa akakubali akaanza kutembea kupitia
ile njia ya mkato,mara akakumbuka ushauri wa
kwanza aliopewa.Akaamua kurudi tena kwenye
njia ya awali ile ndefu Baadae akaja kugundua ile
njia ya mkato ilikuwa na waasi waliokuwa wanaua
yeyote na kumteka akipitia hiyo njia.Akatembea
kwa muda mrefu akachoka
akaona nyumba ya wageni akalipia pesa akaoga
afu akalala.Usiku akasikia makelele sana akaamka
ili akaangalie kuna nini,wakati anataka kufungua
mlango akakumbuka ushauri wa pili,jamaa akarudi
akalala zake.Asubuhi mwenye gest akamuuliza
vipi hukusikia makelele usiku? Jamaa akasema
alisikia ila sikutaka kufatilia sana yasiyonihusu.Mw
enye nyumba akasema wewe ni mtu wa pekee
kutoka salama mana hapa huwa kuna mtu
anatoka usiku anapiga kelele na yeyote
anayetoka nje kushangaa na kutaka kujua nini
kinaendelea huwa anauawa na yule mtu na
kuzikwa kwenye uwanja ule.Jamaa akaendelea na
safari na baada ya safari ya siku nyingi usiku na
mchana akafika nyumbani kwake kwake usiku na
mke wake alikuwa amelala.Alipoch
ungulia kwenye
ufa akaona kuna mtu mwingine wa kiume amelala
pembeni.Jamaa alipatwa na hasira na ghadhabu
akataka aingie awaue mke wake pamoja na yule
mwanaume mwingine aliyekuwepo ndani alafu yeye
arudi akafanye kazi kwa boss wake.Lakini kabla
hajafanya hivyo akakumbuka ushauri wa tatu
akaamua kwanza. Kugonga mlango mke wake
akafungua, hakika mke alifurahi sana akamkumbatia
mume wake.Lakini mume alimsukuma yule
mwanamke na kumwambia ''kwanini
umenisaliti?'' mke akajibu,
“sijakusaliti mume
wangu toka uondoke" Jamaa akauliza “vipi na yule
mwanaume ndani ni nani?".Mke akasema huyo ni
mtoto wako ulipoondoka nilikuja kugundua kuwa
nina ujauzito ndio nikamzaa huyu mtoto".....Wote
walifurahi sana na baadae mke akaandaa chai
ndipo mume akauchukua ule mkate wa tatu
aliopewa na boss.Baada ya sara aliumega mara
akakuta kitita cha pesa nyingi sana,zilizidi hata
zile alizostahili kulipwa baada ya kufanya kazi
miaka ishirini.
Imeandikwa na mwandishi na mtunzi mwalim habelnoah.
MUNGU WETU YUKO KAMA HUYU
BOSS,WAKATI MWINGINE ANAPOTAKA KUJITOA
SADAKA,ANATAKA ATUPE VITU ZAIDI YA VILE
TUNAVYOJITOA,ANATAKA TUWE NA HEKIMA ZA
MUNGU PAMOJA NA BARAKA ZA
MWILINI.MWENYEZI MUNGU ANATUWAZIA MEMA SIKU ZOTE.

No comments:

Post a Comment