Pages

Wednesday, 5 November 2014

GOSBY KUTAMBULISHA "WEMA SEPETU" LEO HII

King Of Swaghili Rapper Gosby leo ame tease mashabiki wake na cover ya single yake mpya kama alivyoahidi, Single hiyo inatarajiwa kutoka leo hii.



 Rapper Gosby aka King of Swaghili kutoka Swaghili Nation leo hii anatarajia kuachia ngoma yake mpya "WEMA SEPETU". Ngoma hiyo imerekodiwa ndani ya  studio za Feel Good Music na imetengenezwa kwa ushirikiano wa producers wawili, Jeffrey kutoka Marekani kwa upande wa midundo na Cjamoker kutoka Tanzania kwa upande wa recording, Mixing and Mastering.


Akiongea na wanahabari Gosby amesema ameamua kushirikisha producers wa nje na wa ndani ya nchi ili kuongeza radha kwenye muziki wake na vilevile kupata uzoefu wa kufanya kazi na watayarishaji tofauti.


“ Muziki wetu unakuwa kwa kasi kubwa, na kama mnavyojua kuwepo kwa mitandao mbalimbali ya kusambaza kazi zetu online inarahisisha sana kazi zetu kufika popote dunia, nadhani ni wakati muafaka sasa tukianza kuangalia soko hili kwa upana zaidi, kuwa na ladha ya bongo na vilevile kuweka ladha ya kimataifa pia"


Akiongea “Wema Sepetu “ Gosby alikuwa na   haya ya kusema


“ Wema Sepetu, dah sijui nianzie wapi ili iwe rahisi kueleweka, anyways.. Wote tunamjua Wema au tumewahi kusikia au kusoma habari kuhusu Wema, Ni former Miss Tanzania, Movies Star, Celebrity wa kike anayezungumzwa kuliko wengine wote ukanda wa Afrika Mashariki, mjasiriamali, Dada Mrembo haswaa!! Wasichana na wanawake wengi wanatamani kuwa Wema Sepetu kwa ujumla au sehemu tu, na huu wimbo umeongelea juu ya msichana au mtoto wa kike ambae labda anafanana na Wema Sepetu .”


Gosby anaendelea

“ Sasa wimbo huu ni special kwa Mawema Sepetu wote ngoja nisimalize utamu, tega sikio leo hii inshallah.....Kwa nini Wema Sepetu mnaweza jiuliza swali hilo, i dont know"


Kaa tayari kwa kazi hii mpya kutoka kwa Gosby

CRD: DAILY MITIKASI BLOG

No comments:

Post a Comment