![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiatUV0oS8dN6fRZuvZpagfkW9QgFtdL-1F7BiBXZ7ZNI9Sa5vl3Ecw8EpMwENDDgwqkzRhymHsUFW1i4sfml1AVqtBLXQqLd9a_gRKWVi3rm8VWbQ_Q3zFwE3_VMc3hNYy2F1Mp-1lvPNU/s320/New+Picture.png)
MKUTANO KUHUSU ADHABU MBADALA YA KIFUNGO GEREZANI KUFUNGULIWA KESHO TAREHE 07 NOVEMBER 2013
Jaji Mkuu wa
Tanzania, Mohamed Chande Othman anatarajiwa kufungua mkutano kuhusu masuala ya
adhabu mbadala wa kifungo gerezani, utakaoanza kesho (6 Novemba, 2013) jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo
umeandaliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Idara ya Huduma kwa
Jamii, kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na
Maboresho ya Sheria za Adhabu la Penal
Reform International, na utafanyika katika Hoteli ya Holiday Inn, Dar es
Salaam.
Lengo la Mkutano huo
ni kujadili masuala mbalimbali kuhusu kuboresha adhabu mbadala wa kifungo
gerezani na pia kupitia maazimio kuhusu
matumizi ya adhabu mbadala yaliyofikiwa katika Mkutano kama huu
uliofanyika nchini Uganda na kuzindua Mtandao unaohusu Adhabu Mbadala wa
Kifungo kwa nchi za Afrika, unaojulikana kama ‘African Alternative to Imprisonnment Network’.
Mkutano huu wa kesho
utakaoendelea hadi keshokutwa, utawashirikisha Wakuu wa Vyombo vinavyosimamia
adhabu mbadala wa kifungo kutoka nchi 10 za Afrika. Nchi hizo ni
Ethiopia, Kenya, Malawi, Rwanda, Afrika Kusini, Sudani ya Kusini, Uganda,
Zambia, Zimbabwe na wenyeji Tanzania.
Mkutano huu ambao
unajulikana kama Mkutano wa Uzinduzi wa Mtandao unaohusu Adhabu Mbadala wa
Kifungo kwa nchi za Afrika (Africa Alternatives to Imprisonment Network
Inaugural Meeting) utafuatiwa na Mkutano mwingine wa Adhabu Mbadala kwa nchi za
Afrika Mashariki (East Africa
Alternantives to Imprisonment
Conference) utaofanyika tarehe 7 hadi 8 Novemba, 2013.
Mkutano huo, mahsusi
kwa nchi za Afrika Mashariki, utawashirikisha wawakilishi wa Idara
zinazoshughulika na Adhabu Mbadala wa Kifungo (Probation and Community Service) na Mashirika ya Kijamii kutoka
nchi za Kenya, Uganda na wenyeji Tanzania. Wafadhili na Mashirika mbalimbali ya
Kimataifa na washiriki wa Mkutano wa Afrika pia wamealikwa kuhudhuria mkutano
huo.
Lengo la mkutano huo
wa nchi za Afrika Mashariki ni kubadilishana uzoefu katika kusimamia
utekelezaji wa Adhabu Mbadala wa Kifungo na kuweka mikakati ya kuboresha
utekelezaji wake kwa nchi za Afrika Mashariki.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
05 NOVEMBA, 2013
No comments:
Post a Comment