Huduma ya kikristo ya Upendo na Furaha Ministry yenye makao yake makuu jijini Dar Es salaam imeanza kutoa msaada na ufadhili wa matibabu kwa watu wanao sumbuliwa na magonjwa na matatizo mbalimbali ya kiafya.
Akifanya mazungumzo na muandishi wa habari hii, Mratibu wa Shughuli za Huduma ya UPENDO NA FURAHA , Mchungaji Ebenezer Mathayo alisema ya kwamba, lengo la huduma hii ni kuwasaidia watu wanao sumbuliwa na magonjwa pamoja na matatizo mbalimbali ya kiafya kupata tiba ya matatizo yanayo wakabili.
Mtumishi huyu wa Mungu aliongeza kwa kusema “ Uchunguzi wetu wa muda mrefu umetuwezesha kugundua kuwa, kuna idadi kubwa sana ya watanzania wanao sumbuliwa na magonjwa pamoja na matatizo mbalimbali ya kiafya ambao wanaendelea kuteseka na matatizo yao kwa sababu ya kutokuwa na uwezo wa kumudu gharama za matibabu ya matatizo ya kiafya yanayo wakabili , katika mahospitali makubwa na vituo mbalimbali vya afya nchini. “
Aliendelea kusema, 'Katika mahospitali na vituo mbalimbali vya afya , gharama za matibabu ni kubwa sana, kiasi ambacho watanzania wa hali ya chini, hawawezi kuzimudu. Bwana wetu Yesu Kristo alituachia amri mpya ya UPENDO, MPENDE JIRANI YAKO KAMA UNAVYO IPENDA NAFSI YAKO'
kama hiyo haitoshi maandiko matakatifu yanaeleza wazi kuwa, inabidi kuwasaidia wagonjwa, yatima, wajane na wenye shida mbalimbali. Sisi kama wakristo tulio mpokea Kristo kama Bwana na Mwokozi wa maisha yetu, tumeitwa na Bwana katika huduma hii ya kuwasaidia wagonjwa na wenye matatizo mbalimbali ya kiafya .
Kama una tatizo lolote la kiafya, na unahitaji kupewa msaada wa matibabu wasiliana nasi kwa simu :0784406508 Au tuandikie kupitia barua pepe: upendonafurahatz@gmail.com.
HABARI KWA HISANI YA MICHUZI JR.
HABARI KWA HISANI YA MICHUZI JR.
No comments:
Post a Comment