Mnyama aina ya Fisi. |
Tukio hilo linalohusishwa na ushirikina, lilitokea Oktoba 27 baada ya Nakuruwa kufariki dunia Oktoba 25 kutokana na kuugua kichwa.
Kabla ya mauti kumkuta alipelekwa kupata tiba katika hospitali binafsi ya Dk Chikumba lakini akazidiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Mkomaindo, Masasi ambako alifariki dunia baada ya muda mfupi na kurudishwa kijiji hapo kuzikwa.
Mwenyekiti wa kijiji hicho, Mawazo Chamanga alimwambia mwandishi wa habari hizi juzi kwamba: "Hapa tumebaki hatuna cha kufanya, kwani limetokea ingawa kwa kijiji chetu jambo kama hili halijawahi kutokea hata kwa mwaka mmoja, ndiyo maana tunashangaa".
Alisema kinachowashangaza zaidi ni kaburi la mtu mzima kuwa na kina kirefu lakini fisi akaweza kulifukua mithili ya binadamu huku akiweka udongo pembeni na kuondoka na maiti bila kuacha hata kipande cha sanda.
"Kama angekuwa fisi wa kawaida asingefukua kaburi hilo wala kuondoka na mwili wa marehemu na badala yake angemtafuna palepale na tungekuta mabaki au sanda," alisema. Mwandishi alifika nyumbani kwa mume wa marehemu, lakini hakumkuta.
No comments:
Post a Comment