Dkt.
Sengondo Mvungi, mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama cha upinzani cha
NCCR-Mageuzi ambaye pia ni Mjumbe wa tume ya Katiba (pichani), amevamiwa usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake jijini Dar es salaam na
amejeruhiwa vibaya kwa kukatwa katwa na mapanga na watu wasiofahamika ambao habari za awali zinadai kuwa ni majambazi.Akithibitisha
tukio hilo, Mkuu wa Idara ya Itikadi na Mahusiano ya Umma wa NCCR-Mageuzi
Taifa, Mhe Moses Machali, ameiambia Globu ya Jamii muda mfupi uliopita kwamba
Dkt Mvungi alijeruhiwa vibaya sana usiku (wa kuamkia leo) saa 6.Mhe
Machali amesema taarifa zilizopatikana ni kwamba walimkata mapanga hasa
kichwani na kumsababishia kupoteza fahamu, na kwa sasa yupo Hospitali ya Taifa
ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu."Wana
NCCR-Mageuzi na Watanzania wote tupeane pole kwa uvamizi wa Dkt Mvungi.
Tumwombee na kumtakia apate kupona haraka", alisema Mhe. Machali, ambaye
pia ni Mbunge wa Kasulu Mjini, akiongezea kuwa hali yake ni mbaya
No comments:
Post a Comment