Mafunzo kuhusu kemikali
Kamati ya mkataba wa kimataifa wa Stockholm unaofuatilia kemikali chafuzi imependekeza kupigwa marufuku kwa matengenezo, matumizi na usambazaji wa aina mbili za kemikali zitumikazo katika kuhifadhi mbao, kwenye rangi na kuua wadudu.
Kwa mujibu wa taarifa ya kamati hiyo kemikali hizo ni PCN na HCBD ambapo kutaka kufahamu hatua zinazochukuliwa na nchi zinazoendelea kujihami dhidi ya madhara ya kemikali hizo, Joseph Msami wa idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa amefanya mahojiano kwa njia ya simu na Mkurugenzi wa mazingira katika ofisi ya makamu wa rais wa Tanzania Dk Julius Ningu anayenza kwa kuelezea mafunzo maalum kwa wataalamu wa viwandani, kilimo na mifugo yanayolenga kujihami na kemikali hizo.
No comments:
Post a Comment