Tuesday, 22 October 2013

RAIS KIKWETE NA MAMA SALMA KIKWETE WATEMBELEA WILAYA ZA WANGING`"OMBE NA MAKETE


  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Paroko wa Kanisa Katoliki wa Parokia ya Kipengere iliyoko katika Wilaya ya Wanging’ombe , Mkoani Njombe wakati Mama Salma alipowasili kijijini hapo tarehe 19.10.2013 akifuatana na Rais Jakaya Kikwete anayetembelea Mkoa wa Njombe.

 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na  wananchi mbalimbali waliofika kuwapokea wakati walipowasili kwenye kijiji cha Kipengere .
  
 
 
Rais Jakaya Kikwete akiteta jambo na baadhi ya Mawaziri aliofuatana nao katika ziara yake ya kuutembelea Mkoa wa Njombe wakati aliposimama katika kijiji cha Kipengere huko Wanging’ombe kukagua mambo ya maendeleo na pia kusalimiana nawananchi
 
 
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na wanachuo wa Chuo cha Ualimu Tandala kilichoko katika wilaya ya Makete , Mkoani Njombe. Mama Salma ameambatana na Rais Jakaya Kikwete ambaye yuko katika  ziara ya siku sita ya kutembelea mkoa huo .
 
 
 
 
Rais Jakaya Kikwete akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi Chuo cha VETA cha Wilaya ya Makete  kilichojengwa katika Mji wa Iwawa, Makao Makuu ya wilaya hiyo. KatIka hafla hiyo uongozi wa Chuo hicho umeamua kukipa jina la Jakaya Kikwete kwa jitihada zake alizowezesha wilaya ya Makete kuwa ya kwanza nchini kuwa na chuo cha VETA cha wilaya. Kulia kwa Rais Kikwete ni Waziri wa Elimu NA Ufundi Dr. Shukuru Kawambwa na kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Makete Ndugu Josephine Matiro.
 
 
 
Rais Jakaya Kikwete akifuatana na Mkewe Mama Salma wakitembelea Chuo cha VETA cha Makete  na kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na wanachuo wa chuo hicho mara tu baada ya kukizindua rasmi
 
 
 
 Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma wakipata maelezo ya namna gani ya kupata udongo unaofaa kwa ajili ya kufyatua matofali kutoka kwa  Geofrrey Sanga na Abel Mbilinyi, wanachuo  wa mwaka  wa kwanza wa chuo hicho
 
 
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea zawadi ya kikapu kutoka kwa mama Janeth Luvanda  anayewawakilisha akinamama wazee wa wilaya ya Makete wakati wa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Rais Kikwete katika Mji wa Iwawa, Makao Mkauu ya wilaya ya Makete
 
PICHA NA JOHN LUKUWI. 
 

No comments:

 

ADVERTISE WITH US

AFRICAN FASHION

PLACE YOUR ADS HERE!