Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwaeleza waandishi wa habari jinsi utafiti wa Gesi na mafuta unavyofanyika baharini muda mfupi baada ya kuzindua awamu ya nne ya Utafiti wa Gesi na mafuta uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.Rais Kikwete aliwahi kuingoza wizara ya Nishati na MadiniRais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akibonyeza kitufe kuashiria Uzinduzi wa Mkutano wa Nne wa Kugawa Vitalu vya Utafutaji Mafuta na Gesi Baharini katika Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Professa Sospeter Muhongo na kulia pembeni ya Rais ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPDC Mhandisi Joyce Kisamo.
………………………………………………………………………………………….
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
RAIS Jakaya Kikwete amesema uwekezaji katika sekta ya mafuta na gesi utakuwa kwa manufaa ya Watanzania na hakuna hasara itakayopatikana kulingana na, Sheria mkataba wa ubia na mfumo wa sasa uliopo.
Kauli hiyo ilitolewa leo na Rais Kikwete wakati wa uzinduzi wa awamu ya nne ya ununuzi wa leseni za uchimbaji wa vitalu vya mafuta na gesi uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu J.K. Nyerere jijini Dares Salaam, ambapo alisema kumekuwa na mabishano mengi katika jamii kuhusu mfumo wa sasa juu ya jambo hilo kwamba Watanzania hawanufaiki, bali wanaonufauika ni kampuni zinazowekeza wakati suala hilo halina ukweli.
“Anayesema tunatapata hasara hajuwi ukweli ,kama anajua anapotosha ukweli,” alisema Rais Kikwete.
Rais Kikwete alisema sheria ya sasa inashirikisha Shirika la Maendeleo ya Mafuta Tanzania (TPDC) na kampuni za mafuta na gesi ,ambapo kampuni ndizo zinagharamia uwekezaji na kutafuta.
Aliongeza kuwa gharama za kuchimba kisima kimoja ni karibu dola za Kimarekani milioni100, hivyo kampuni hizo zitakapokuwa zinauza zinaruhusiwa kurudisha gharama zao zilizotumika.
“Baada ya miaka mitano au 10 ijayo gesi itaanza kuuzwa. watakapokuwa wanauza wanaruhusa ya kulipa gharama zao. Tutagawana mapato mfano TPDC watapata asilimia 65 au 75 na kampuni zitapata asilimia 35 au 25 ,alisisitiza Rais Kikwete huku akihoji kuwa kuna ubaya gani?
Rais Kikwete alifafanua kwamba kuhusu hoja ya sekta binafsi kushirikishwa katika uwekezaji huo, alisema bado kuna umuhimu wa kuwashirikisha.
“ Ninataka niwahakikishie hakuna ubaguzi katika uwezekezaji wa jambo hili. Watanzania wakiweza kuwekeza katika suala hili itakuwa ni kwa masharti hayahaya, lakini shughuli hii ina ghali. Hivyo jambo la kungalia ni namna gani? Tutamsaidiaje mzawa haya tutazungumza.
“Kama kuna namna ya kumsaidia tuzungumze, tusilaumIane kama mtu na maoni tuko tayari sisi kuyasikiliza” alisema.
Aidha Rais Kikwete alisema kuhusu kuwatengea maeneo wazawa ni jambo gumu kwa kuwa hakuna mtu mwenye uhakika eneo fulani lina mafuta au gesi.
Aliongeza kuwa Serikali inachokifanya sasa ili kuhakikisha maslahi ya Watanzania yanalindwa ni kujenga uwezo wa ukaguzi ili mtu anaposema hajalipa gharama zake za uwekezaji au amepata ujazo wa cubmita tisa iwe ni kweli.
“Tulifanya hivyo katika sekta ya madini tukaweza.Tutawakagua kwa maarifa tuliyotumia katika madini”, alisisitiza huku akisema Serikali itafanya kazi wa kuwafundisha watalaamu wa ukaguzi, wapimaji wa mafuta na gesi na wahandisi.
Alisema kuhusu Serikali kuwepo katika uwekezaji huo au sekta binafsi iingie jambo hili litabidi lijadiliwe kwa kuhusisha pande zote.
Rais Kikwete alizitaka kampuni zitakazohusika katika uchimbaji huo kuzingatia sheria ya uhifadhi wa mazingira wakati wa uchimbaji huo ili kulinda maliasili za nchi. Pia alizitaka zifahamu kwamba mahitaji ya gasi yapo Tanzania na nje ya nchi.
Kwa upande wake Waziri wa Nishati na Madini,Profesa Sospeter Muhongo alisema sera ya usimamizi wa mafuta na gesi imeshakalimika na itakuwa katika lugha ya Kiswahili na Kiingereza.
PICHA NA FRED MARO.
No comments:
Post a Comment